Eric Omondi akamatwa na kanju akiendesha kigari chake katikati mwa jiji Nairobi

Kigari chake kilikuwa kinavutwa huku Eric akiwa ameketi kwenye kigari hicho na askari wa kanju walikuwa wanamzingira wakielekea kituoni.

Muhtasari

• Askari wa manispaa ya kaunti ya Nairobi maarufu kama Kanju walimkamata akiendesha kigari hicho jijini na kumzingira.

• Baadae waliita gari lao la kuvuruta magari yaliyokamatwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha Central.

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: Instagram

Licha ya kuwa baba mpya kabisa mjini, mchekeshaji Eric Omondi hajaacha vituko vyake vya kuchekesha.

Mchekeshaji huyo ambaye hivi karibuni amelekeza nguvu nyingi katika harakati za kupambania haki za kibinadamu kwa mara nyingine tena ameonekana kukamatwa katikati ya jiji la Nairobi aliendesha kigari chake ambacho kina muonekano wa kiatu kikubwa.

Eric alipakia klipu hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo askari wa manispaa ya kaunti ya Nairobi maarufu kama Kanju walimkamata akiendesha kigari hicho jijini na kumzingira.

Baadae waliita gari lao la kuvuruta magari yaliyokamatwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha Central.

Kigari chake kilikuwa kinavutwa huku Eric akiwa ameketi kwenye kigari hicho na askari wa kanju walikuwa wanamzingira wakielekea kituoni.

“Tafadhali tuache Ubaguzi, Magari yote yanastahili heshima😡😡😡😡😡😢😢😢😢😢 🤦‍️🤦‍️” Eric aliandika kwenye klipu hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake walihisi mchekeshaji huyo alipanga tukio hilo kwa faida yake na wengine hata kuibua maswali ni muda gani huwa anakaa na mtoto wake mchanga Kyle ambaye hana hata wiki tangu kuzaliwa.

“Unamtunza mtoto Kyla saa ngapi 😂😂😂😂😂😂 huwa uko busy mbali na nyumbani,” Diana Marua alimuuliza.

“Kwani wamekushika tena,” Ngami Moses alimuuliza.

“Eric Omondi arrested again 😂😂😂😂😂😂😂😂kwani pia kuendesha gari yakoo unashikwa,” mwingine aliuliza.

‘Hauchoki na hiki kiatu😂😂😂’