Ngesh Kaveve Kazoze: Mimi sijakataa Stevo Simple Boy lakini…

Stevo alimtaka kutambua kuwa wengi wao ni wale wa kumchezea na kutaka kuteleza kwa ganda la ndizi kwa umaarufu wake, akijipigia debe kwamba yeye ndiye pekee mwenye nia nzuri naye.

Muhtasari

• “Yangu hata sijui kama itafunguka sasa hivi. Yangu iko kidogo tu, funguo moja tu ifunguke,” Ngesh alijibu.

Kaveve Kazoze na Stevo
Kaveve Kazoze na Stevo
Image: Instagram

Rapa chipukizi wa kundi la Spider Clan Ngesh wa Vasha maarufu kama Kaveve Kazoze kwa mara nyingine amepiga pasi uvumi kuhusu msanii Stevo Simple Boy kumtaka kimapenzi.

Katika video moja ambayo imeenezwa mitandaoni, Ngesh amekiri kwamba hajamkataa Stevo Simple Boy ila tu anakumbwa na kizingiti kimoja.

Ngesh anasema kwambac Stevo Simple Boy licha ya kutaka, anatambua kwamba ni mume wa mtu na asingependa kumsababishia uchungu mwanamke mwenzake na hivyo kumtaka msanii huyo wa Kibera kuganda katika penzi la mke wake.

“Mimi sijamkataa Stevo Simple Boy lakini wacha tu atulie na bibi yake maze…” Ngesh alisema kabla ya Manzi wa Kibera kumkatiza akimwambia kwamba anambutua komborera la moyo Stevo Simple Boy.

Manzi wa Kibera alimuuliza kiasi cha mahari ambayo angependa kutolewa na mwanamume yeyote ambaye angependa kumchumbia na nia ya kumuoa na Ngesh alijibu;

“Yangu hata sijui kama itafunguka sasa hivi. Yangu iko kidogo tu, funguo moja tu ifunguke,” Ngesh alijibu.

Ngesh anamjibu Stevo Simple Boy siku moja tu baada ya Stevo kujitokeza akisisitiza kwamba angependa kupata muda angalau kidogo kuzungumza naye ili kupata mwafaka kuhusu ombi lake la kumtaka kimapenzi.

Stevo alisema kwamba japo anaelewa kuna wanaume wengi wanaomtaka Ngesh, lakini mrembo huyo anafaa kutambua kuwa wengi wao ni wale wa kumchezea na kutaka kuteleza kwa ganda la ndizi kwa umaarufu wake, akijipigia debe kwamba yeye ndiye pekee mwenye nia nzuri naye.

“Ngesh ni msichana mrembo, mtoto ameumbika, unaona. Lakini akuje kwangu ili tuongee tuone kama tunaweza toka kimapenzi na mambo yakiwa sawa mimi nitawaambia Wakenya ndio huyu. Pia anafaa afikirie kwamba sasa hivi kuna wanaume wengi wanamtaka lakini kuna wale pia wanakuja kudandia huo umaarufu wake, mimi nitamwambia Kaveve Kazoze ninampenda kisha wamuachilie,” Stevo alisema.