Karen Nyamu adokeza hakuna mwanamke ataepuka ndoa ya wake wengi mume akiamua

Nyamu alimjibu shabiki mmoja kwa kauli inayoweza kutafsiriwa kwamba wanawake wengi wanaowacheka wenzao walioko kwenye ndoa ya wake wengi wanadhani wao wataikwepa ndoa ya aina hiyo.

Muhtasari

• Samidoh aliachia wimbo mpya akimshirikisha Joyce Wa Mamaa wenye maudhui ya kumbembeleza mkewe kutoivunja ndoa yao.

• Wengi walihisi msanii huyo anamuimbia Edday na kumtaka kurudi nyumbani.

Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Image: Instagram

Seneta maalum Karen Nyamu kwa mara nyingine amewaacha mashabiki wake katika njia panda baada ya kumjibu shombo shabiki mmoja aliyesifia wimbo mpya wa Samidoh ambao inasemekana amemuimbia mke wa kwanza Edday Nderitu.

Karen alipakia picha yake nzuri kawaida kwenye kurasa zake mitandaoni akiwahimiza wafuasi wake kutolaza damu na badala yake kuchapa kazi kwa bidii.

Hata hivyo, wengi hawakuonekana kuzingatia ujumbe wake, na badala yake walionekana kumchombeza na kumhasi kwa kutaka kusikia maoni yake kuhusu wimbo mpya wa baba watoto wake wawili – Samidoh.

Shabiki mmoja alimchokoza Nyamu akitaka kujua kama ameusikiliza wimbo huo wa Mugithi, na kwenda mbele hata Zaidi akiusifia kwamba ni wimbo mtamu ambao umetumika kama ujumbe wa kumbembeleza Edday Nderitu kurudi nyumbani baada ya kukaa Marekani kwa muda mrefu.

“Umeskiza wendo witu by Samidoh akiimbia Eddy, I love the vocals,” mtumizi wa Facebook Njambi Wa Dee alimuuliza Karen Nyamu kwenye sehemu ya kutoa maoni.

Nyamu alimjibu kwa shombo katika kauli ambayo inaweza fafanuliwa kwamba wanawake wengi wanamcheka wakidhani wao watakwepa ndoa ya wanawake wengi.

Njambi Wa Dee Polygamy bado mnaona mkiepuka lol,” Karen Nyamu alimujibu.

Wimbo mpya wa Samidoh Wendo Witu una maudhui ya mwanamume ambaye anamuimbia mke wake baada ya kukosana na kutishia kuondoka nyumbani na kuivuruga ndoa.

Katika wimbo huo, Samidoh anambembeleza mama watoto wake akimtaka kutochukua uamuzi wa kuondoka nyumbani na badala yake kuketi chini na kukumbuka umbali ambao wametoka pamoja kama wanandoa.

Ujumbe huu kwenye wimbo huo uliwafanya wengi kuhisi kwamba ni ujumbe kwa njia ya wimbo ambao alitaka umfikie mama wa watoto wake Edday Nderitu ambaye yuko Marekani kwa miezi kadhaa sasa, bila kuonesha dalili yoyote ya kurudi Kenya.

Wiki chache zilziopita, Edday aliandika ujumbe wa kunyoosha maelezo kwenye Facebook akisema kwamba aliamua kumuacha Samidoh mikononi mwa mwanamke [Karen Nyamu] ambaye alikuwa na haja kubwa ya kukaa naye, na kwamba yeye asingekaa na kuanza kumpigania Samidoh.