Inauma-Rayvanny awapasha mapromota baada ya shoo yake kufeli Goma,DRC

Alikiri waziwazi kuvunjika moyo, kwani nafasi aliyokosa ilimzuia kushiriki matukio muhimu na mashabiki wake.

Muhtasari
  • Rayvanny alieleza kusikitishwa kwake na kusema kwamba mapromota hao walipuuza kumfikia hotelini kwake ili kuzungumzia mambo muhimu kabla ya onyesho hilo.
CEO wa Next Level Music
Rayvanny CEO wa Next Level Music
Image: Facebook

Msanii wa Bongo Flava kutoka Tanzania Rayvanny kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram aliwakashifu mapromota wake wa Goma, DRC baada ya kuchangia pakubwa katika kufeli kwa shoo yake.

Rayvanny alieleza kusikitishwa kwake na kusema kwamba mapromota hao walipuuza kumfikia hotelini kwake ili kuzungumzia mambo muhimu kabla ya onyesho hilo.

"GOMA PROMOTERS @happy_people_drc !!!!! WATU WAMEKUJA KUNIONA NA MUMESHINDWA KUNIFATA HOTELINI HADI MUDA HUU WATU WAMESUBIRI HADI WAMECHOKA NA FUJO ZIMETOKEAA HADI SHOW IMEHARIBIKA INAUMA SANA KWA NINI????? !!!!,"Vanny aliandika.

Rayvanny aliendelea kueleza uchungu aliokuwa nao kutokana na kufeli kwa shoo hiyo, licha ya maandalizi yaliyokuwa yamefanyika kwa umakini.

Alikiri waziwazi kuvunjika moyo, kwani nafasi aliyokosa ilimzuia kushiriki matukio muhimu na mashabiki wake.

Alichukua nafasi hiyo kuwahakikishia wafuasi wake kwamba ana upendo mkubwa kwao.

NAJISKIA VIBAYA KWA NINI MMESHINDWA KUACHA NIFURAHI NA WATU WANGU ???? 😭😭😭😭😭😭😭 NAWAPENDA#GOMA 🇨🇩🇨🇩🇨🇩 I FEEL SOOOOOOO BAD."

Katika sehemu ya maoni, mashabiki wake walimwonea huruma kutokana na tukio hilo la bahati mbaya, huku baadhi wakimtupia lawama kwa kushindwa kufanyika kwa shoo hiyo mjini Goma.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki wake;

silencia: Siungechukua boda uchomoke uende braza

saudi: Papaa poye sana, wakuye kwa hotel kukupick, ukachape mangoma ba watu ba goma batatulie na kufughai

mchilijac: Dah nimelia sana wameninyamazisha watu hadi wamechoka😭😭

hemedi: Makosa ni yako @rayvanny umetu kosea mashabiki zako wa Goma😭😭😭 ume acha ajali nyingi zime tokea apa mjini Goma

sumaili: @frontdee mwenyewe maskini sisi tuna hela ndio maana mume fika apa Goma!! I love ❤️ Goma !! Ak 47 una fasmu mulio yayo wewe🔥