Yemi Alade asimulia jinsi alinusurika kifo baada ya kuhusika katika ajali

"Mnamo tarehe 17 Agosti, tulikuwa kwenye ajali ya gari, mahali fulani kati ya barcelona na benicassim nchini Uhispania

Muhtasari
  • Msanii huyo mwenye umri wa miaka 34 alizidi kumshukuru Mungu kwa bahati yake ya kunusurika.
Yemi Alade
Yemi Alade
Image: Hisani

Mwanamuziki kutoka Nigeria Yemi Eberechi Alade amesimulia jinsi alivyonusurika katika ajali ya gari nchini Uhispania.

Msanii huyo maarufu wa kibao cha  "Johnny" aliingia kwenye Instagram Jumanne akidai kwamba mnamo Agosti 17 alihusika katika ajali ya gari mwendo wa saa 12:06 jioni mahali fulani kati ya Barcelona na Benicassim.

"Mnamo tarehe 17 Agosti, tulikuwa kwenye ajali ya gari, mahali fulani kati ya barcelona na benicassim nchini Uhispania saa 12:06(mchana)pia nilipatwa na dharura ndogo ya matibabu kutokana na uchovu baada ya kutumbuiza kwenye jukwaa saa 7 baada ya tukio siku hiyo hiyo.na kwa namna fulani, niliishia kwenye "after party"πŸ€―πŸ€­πŸ’ƒ(niache o. akili yangu ilihitaji mitetemo chanya)

Maisha ni ya walio hai... Sikutaka kuliweka hili wazi, lakini shetani alikuwa na mipango mingine, lakini Yehova jiray wangu alisema HAPANA!DAMU ya Yesu ilinena kwa ajili yetu.Nilipoteza kucha tu, yote yalitokea ghafla,"Yemi alisimulia.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 34 alizidi kumshukuru Mungu kwa bahati yake ya kunusurika.

"DAMU ya Yesu ilinena kwa ajili yetu.Hakuna jambo la ghafla au gumu kwa Mungu.Neema yake inatosha."

Hakuna majeruhi walioripotiwa.

Mashabiki walimfariji na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

josh: The Bible said that a thousand at thy left hand side and ten thousand at thy right hand side they shall do their evil but it will never come close to the children of God.. You protected Momma. I'm glad nothing happened love you

tiwasavage: The devil is a liar. May God continue to protect you πŸ™πŸΎ

prom: My God! Thank God for his protection over your lifeπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ”₯πŸ”₯

ireri: πŸ™Œ you're the winner πŸ† and always πŸ«‚ love from Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ i