Harmonize amchana Khaligraph Jones kwa kuwadharau marappa wa Tanzania

Katika stori zake za Instagram, Harmonize alimkashifu Khaligraph kwa kile alichokiona kama dharau ya wazi dhidi ya vipaji vya Kitanzania.

Muhtasari
  • Harmonize alizidi kumdokezea rapa nguli, Profesa Jay, na kusisitiza kuwa Khaligraph alikuwa mbali na kufikia hadhi ya marappa wakubwa wa Tanzania kama yeye.
Harmonize.
Harmonize.
Image: Instagram

Mwimbaji Harmonize amemjibu Khaligraph Jones baada ya kuwashambulia marapa waTanzania na  kuizua mjadala mkali.

Mzozo huo ulianza pale Khaligraph Jones alipojitangaza kwa ujasiri kuwa bingwa wa kufoka wa Kenya na Nigeria ambaye hashindaniwi na mpinzani wake, huku akiwaangusha rappas wa Tanzania.

“Watanzania rappers wenu wana saa 24 za kujibu. Nikikosa nitafanya shambulizi na nitatwaa tasnia nzima ya muziki wa Tanzania na kuwa rapa bora zaidi Tanzania kama vile mimi ni rapa bora zaidi Nigeria na Kenya,” Khaligraph alisema kwa kujigamba.

Katika stori zake za Instagram, Harmonize  alimkashifu Khaligraph kwa kile alichokiona kama dharau ya wazi dhidi ya vipaji vya Kitanzania.

Katika majibu yake, Harmonize alikosoa msimamo wa Khaligraph, akisisitiza kwamba rapper huyo mwenyewe alipata msukumo kutoka kwa wasanii wa kufoka wa Tanzania.

"Jinsi nilivyojitolea kwa bidii kukupa tuzomwaka huu sikujua unaweza jihisi mkubwa hivyo na kuwadharau ndugu zangu. You really know all your rap inspiration its from TZ bro dont forget home!" aliandika.

Harmonize alizidi kumdokezea rapa nguli, Profesa Jay, na kusisitiza kuwa Khaligraph alikuwa mbali na kufikia hadhi ya marappa wakubwa wa Tanzania kama yeye.

Alisisitiza madai ya OG kwa kurejelea ushirikiano wake, akisisitiza kwamba alikuwa bado hajatimiza.

"Unawajua Weusii, vipi kuhusu baba yako Profesa Jay level yako ni Lunya na Con Boy county boy na bado wanakulalisha!! Unaweza kusema kupitia kolabo zako. OG relax, TZ hip hop ni level nyingine!" Harmonize alieleza kwa ukali.