Huwa nachora tattoo za Ex wangu wakiaga dunia-Shakilla akiri

Kauli hiyo imezua mijadala mingi huku wengi wakihoji ni wangapi kati ya wake waliofariki dunia.

Muhtasari
  • Aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kusema kwamba huwa anachora tattoo hizo baada ya kuchumbiana na wanaume hao na wakiaga dunia.
Image: INSTAGRAM// SHAKILLA

Mwanasosholaiti wa Kenya Shakila aliwaacha wengi kwa mshangao baada ya kukiri kuwa na tattoo 19.

Aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kusema kwamba huwa anachora tattoo hizo baada ya kuchumbiana na wanaume hao na wakiaga dunia.

Kauli hiyo imezua mijadala mingi huku wengi wakihoji ni wangapi kati ya wake waliofariki dunia.

Kujibu udadisi huu, alisisitiza tattoos zilitokana na kifo cha mtu mmoja, ex wake wa kwanza.

Akizungumza na blogu za ndani, alishiriki

"Nina tattoo 19 kwa jumla 11 ni za ex wangu. Nilichora tattoo yangu ya kwanza mara tu baada ya ex wangu kufariki. Tattoo iliyonitia moyo zaidi, niliyokuwa nayo ni ya uso wa rafiki yangu wa karibu. Ninachora wapenzi wangu wa zamani wanapofariki. "

Baada ya ufichuzi wake Shakilla wanamitandao walikuwa na haya yan kusema;

kenyan g: The mediocrity we praise in this country is amazing. Anyway, in a few years the topic will change to "everyone has a past and shouldn't be judged. I have experienced growth and salvation" lmao

afrique: Death doesn't necessarily mean mortal..😂😂

frash: Kenyan journalism, smh.. ati "any message you have for someone who's planning to have a tattoo? 🗑🚮

steve: Weeeh does she date sick people? Coz hizo deaths za ma ex

chris: This is also cult why tattoo's of them when they died while they were alive you could do😢