Mamake Zuchu ageuka mbogo kwa Mwijaku kisa kumshauri kuhusu kuzini kabla ya ndoa

Mwijaku alijaribu kumshauri Khadija Kopa kumkanya bintiye Zuchu dhidi ya kutoka kimapenzi na Diamond kabla ya ndoa rasmi ya Nikkah lakini Kopa akawa mbogo na kumzima Mwijaku kwa maneno makali.

Muhtasari

• Zuchu na Diamond wamekuwa wakisemekana kutoka kimapenzi kichini chini na hata kuitana mke na mume licha ya kwamba hawajafunga ndoa rasmi.

Mwijaku na Kahdija Kopa.
Mwijaku na Kahdija Kopa.
Image: Instagram

Mamake msanii Zuchu, Bi Khadija Kopa amemkoromea vikali mtangazaji mbwatukaji Mwijaku baada ya mtanagzaji huyo kuonekana akifanya mahojiano na kuzungumzia kuhusu suala la Zuchu kuzini kabla ya ndoa.

Mwijaku alimshauri Khadija Kopa kuishika dini na kumkanya binti yake dhidi ya kujihusisha kimapenzi na bosi wake Diamond Platnumz kabla ya kuoana rasmi na kupata Baraka za Allah kwa mujibu wa sheria za dini ya Kiislamu.

Hata hivyo, Mama Khadija Kopa aligeuka mbogo kwa ushauri huu wa Mwijaku akimtaja kama mtu mnafiki sana ambaye hana heshima kwa wanawake.

Wewe hukusoma, dini gani imesema umdhalilishe mwanaadamu mwenzio kwa njia yeyote wewe nimdhalilishaji wa wanawake mpaka picha za utupu umetuma kumdhalilisha leo unajifanya unajuwa dini nijibu kwa aya aya gani imesema umdhalilishe mtu. Nilikwambia nataka mtu azini nimekwambia ndoa unaona dilili kwani mtu huolewa na Alieandikiwa naye nani anae taka mtoto wake azini wewe unakipwate unajiona wewe peke yako hapa duniani uko sawa wakati unayoyafanya huyaoni unayafumbia macho kwa kuwatolea wenzio maneno ya karaja unajifanya unachekesha unafikiri watu wanapenda unaowafanyoa au hujasikia atemdhalilisha mwenziwe naye atadhalilishwa mara mia moja,” Kopa alimpa mzomo.

Mwijaku alimjibu akiwambia kwamba yeye anaongea kama sauti ya busara itokayo kwa Mungu, akijipiga kifua kwamba yeye ni msomi mwenye digrii mbili na pia mwenye ufahamu mkubwa kuhusu dini, akisisitiza kwamba hakuna aya hata moja kweney Quran ambayo inahimiza uzinifu.

Kopa alimibu akimwambia kwamba ni kiherehere cha njaa tu ndicho kinamfanya kubwatuka maneno ya hovyo ilimradi apate cha kutia kinywani.

Kopa pia alimwambia Mwijaku kwamba hata yeye ana mtoto wa kike na anasubiri sana wake akue ili amuonee jinsi atakavyowalea kwenye maadili hayo ya Kidini anayomwambia.

“Hukutaka kunifundisha ulitaka kunidhalilisha kama ulitaka kunifundisha si tunakutana siungenambia mbona hujanambia umekwenda kukaa kwenye waamdishi unidhalilishe alama za mnafiki hizo nawewe unazo. Unachekesha sana unayo mtendeya mwenzio nawewe yatakufika omba mungu akunusuru dunia ndo hiihii mamaako hakuomba kuwa na mtoto usohaya kama wewe,” aliongeza Kopa.