Mume wako Brown Mauzo ni beach boy, alikuvisha pete feki ya almasi - Shakila kwa Sidika

Vera Sidika alimjibu Shakilla akimwambia kuwa yeye hajatulia ndio maana kaitka mwaka wa 2023 peke na ambao bado hujaisha tayari ameshatoka kimapenzi na wanaume zaidi ya 100.

Muhtasari

• Shakilla pia alipiga madai mengine akisema kuwa pete ambayo Mauzo alimvisha Vera walidanganya kuwa ilikuwa ya almasi lakini akasema kuwa ni almasi ghushi.

Shakilla amshambulia Vera Sidika, Brown Mauzo atajwa
Shakilla amshambulia Vera Sidika, Brown Mauzo atajwa
Image: Instagram

Wikendi iliyopita, wanasosholaiti Vera Sidika na Shakilla wamekuwa wkaiparuruana kwa maneno makali haswa baada ya mwanasosholaiti Shakilla kumtaka Vera Sidika kustaafu akisema wanawake wanaisha muda wao sokoni wakiwa na miaka 28.

Tamko hilo lilionekana kumghasi Vera Sidika ambaye alijibu katika kile amabcho anajua kukifanya vizuri, lakini naye Shakilla alishikilia msimamo wake na mashabiki walipata fursa nzuri ya kuona mashambulizi hayo.

Shakilla alimpiga Sidika kumbo chini ya kitovu kwa kumwambia kwamba aliona amekwamba na hakuna mtu aliyekuwa tayari kumfuatilia hadi akaamua kutulia na msanii Brown Mauzo ambaye Shakilla alimtaja kama kijana wa ufukweni.

 Shakilla pia alipiga madai mengine akisema kuwa pete ambayo Mauzo alimvisha Vera walidanganya kuwa ilikuwa ya almasi lakini akasema kuwa ni almasi ghushi.

“Akiwa na haya makalio yote akidanganya kuwa aliwahi kula pamoja na akina Kardashian na mbona basi baadae aliishia kutulia na beach boy ambaye alimpa pete feki ya almasi,” Shakilla aliandika.

Akimjibu, Vera Sidika alimwambia kwamba yeye tayari ameshatumika sana na hana haja ya kusubiri hadi afike miaka 28 ili kustaafu kutoka kuwa mwanasosholaiti.

Sidika pia alimpiga vikali akisema kwamba Shakilla amekuwa akiwadanganya watu kuhusu umri wake kuwa ni miaka 20 akimsuta vikali kwamba katika umri huo wake tayari ameona mengu kuliko umri wake.

“Katika mwaka wa 2023 pekee huyu tayari ameonana na wanaume 100, si kushangaa kwamba katika umri wa miaka 20 tayari maziwa yake yameporomoka kama makubadhi ya bafuni,” Sidika alimwambia huku akiwambia kuwa asingedhubutu kuanzisha vita ambavyo alikuwa anajua haviwezi, huku pia akisema kuwa Shakila alikuwa anatafuta umaarufu kupitia kwake.