Nyimbo zaidi ya 500 zimetolewa Tanzania kunitusi, zingine 10,000 ziko studioni - Khaligraph

“Pale kwa trending Tz tayari kuna nyimbo zaidi ya kumi za ndugu Omollo, Hip Hop kaamka vile yapaswa, The OG has been Respected,” aliongeza.

Muhtasari

• Khaligraph alisema kuwa lengo lake la kuamsha popo za wasanii wa rap Tanzania limetimia kwani sasa hivi yeye ndio gumzo.

Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: Screengrab

Ikiwa ni siku chache baada yakuwaamksha popo wasanii wa rap kutoka Tanzania, msanii wa humu nchini Khaligraph Jones sasa anadai kwamba wasanii hao wameingie studioni na ubaya na kurekodi ngoma Zaidi ya 500 za kumtukana yeye.

Jones wiki jana alifanya video akiwashtumu vikali wasanii wa HipHop nchini Tanzania akisema kwamba wamelala na kwa sasa hakuna anayeweza kumpa changamoto hata kidogo kwenye ulingo wa kutema mistari.

Alifanya ngoma akiwadhihaki vikali na kusema kwamba amewapa saa 24 tu kumjibu iwapo wanaona wako tayari kuenda sawa na yeye kwenye ubabe wa kutema maneno yenye vina vya tafsiri.

Kabla hata ya siku saba kupita, Jones amedai kwamab nchini Tanzania sasa kila msanii wa rap amejikung’uta mavumbi na anataka kujionesha na ubabe wake wa kutunga maneno ya rap akisema tayari nyimbo 500 za kumtukana zimeshatoka na zingine Zaidi ya elfu 10 ziko studioni ndio mwanzo zinakarabatiwa kabla ya kutoka.

Ripoti napata ni kwamba pale Bongo Kuna Nyimbo zaidi ya elfu tano zinazomtusi OG na zingine elfu Kumi zipo kwenye studio zinapangwa kutolewa wiki ijayo,” Khaligraph alisema.

Msanii huyo ambaye juzi aliwataka wasanii hao kuenda pole pole kwa kile alisema kuwa alikuwa anataka kuwachangamsha alisema kuwa lengo lake limetimia kwani Tanzania upande wa trending ni nyimbo zinazomzungumzia yeye.

“Pale kwa trending Tz tayari kuna nyimbo zaidi ya kumi za ndugu Omollo, Hip Hop kaamka vile yapaswa, The OG has been Respected,” aliongeza.