Samidoh aahidi kufuata nyayo za msanii mwenzake wa Mugithi mwenye wake wawili

Samodoh alifunguka ukweli huo katika hafla ya kitamaduni ambapo rafiki yake alikuwa anatoa mahari kwa mke wake wa pili na kusema hakuna maisha mengine kando na ya kuishi na wake wawili.

Muhtasari

• Samidoh ana watoto watatu na mke wa kwanza Edday Nderitu na wawili na babymama Karen Nyamu.

Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Image: Instagram

Afisa wa polisi ambaye pia ni msanii wa Mugithi Samidoh amesisitiza kwamba maisha yake ni sharti aishi katika ndoa ya wanawake wawili.

Alizungumza haya wakati wa hafla ya kutoa mahari kwa mke wa pili wa msanii mwenzake wa Mugithi Mwigai wa Njoroge wikendi iliyopita.

Samidoh, ambaye amekuwa katika ndoa na Edday Nderitu kwa miaka 15 na ana babymama, Karen Nyamu, alitumbuiza katika harusi ya kitamaduni ya Muigai na Quen Stacey mnamo Jumamosi, Agosti 26.

Huku akitumbuiza katikakati ya umati mdogo, msanii huyo alipewa nafasi ya kuongea ambapo alishika kipaza sauti na kuongea kwamba hakuna mkondo mwingine kwake Zaidi ya kufuata mfano ambao umeoneshwa na Muigai wa Njoroge – mfano wa kuwalipia mahari wanawake wake wawili Edday Nderitu na Karen Nyamu.

“Kwa hakika nyayo za Muigai ni kama hizi tu kwa sababu maisha ndio kama haya,” Samidoh alisema kabla ya kupokezana kipaza sauti na kutoroka jukwaani kwa tabasamu pana usoni.

Licha ya kuweka wazi kufuata nyayo za ndoa ya mitala, itakumbukwa mkewe Edday Nderitu kabla ya kuelekea Marekani aliandika ujumbe mrefu mwezi Mei mwaka huu akisema kwamba hata siku moja hawezi kukaa kwenye ndoa ya mke Zaidi ya mmoja ili kuwalea watoto wake.

Baada ya kufika Marekani, hivi majuzi Nderitu alipiga pale pale kwenye mshono akisema kuwa aliamua kuwapeleka watoto wake mbali na Samidoh ili kuwaepusha kutokana na athari za kisaikolojia ambazo zingewakumba kutokana na mgogoro wa kimapenzi baina ya wazazi wao na babymama Karen Nyamu.

 

Hii hapa ni video ya Samidoh akiongea kuhusu kufuata nyayo za mwenzake;