Stevo adai vipusa wa Tanzania wamefurika DMs zake baada ya kusikia ni mkali kwa rap

“Wanadada wenyewe tu ndio wananipenda kwa sababu mimi ni mtanashati, niko wa moto na mimi ni mtamu, wanahisi wakifanya mapenzi na mtu maarufu kama mimi wanahisi vizuri," Stevo alisema.

Muhtasari

• Stevo alisema kuwa wanadada wengi wanampenda kwa kile alisema kuwa yeye ni wa moto asiyeweza kuepukika.

• Msanii huyo alifichua kwamba mke wake wa sasa hivi ni raia wa Tanzania ambaye alimpata kwa njia hiyo hiyo ya kumvizia kwenye DM.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Screengrab

Msanii Stevo Simple Boy amedai kwamba warembo kutoka taifa jirani la Tanzania wamefurika kwenye DMs zake baada ya kusikia kwamba ni mkali katika muziki wa kutema madini na hawezi ushindanishwa na rapa hata mmoja kutoka Tanzania.

Stevo alifichua madai haya katika mahojiano na wanablogu wa habari za mitandaoni akisema kwamba DM zake sasa hivi hazitulii kwani kila mara anapoingia kwenye mitandao yake ya kijamii anaona watu wengi wasichana kutoka Tanzania kwenye DM wakimtaka kuwakubalia kutoka naye kimapenzi.

“Vichuna wa Tanzania wamejaza DM yangu wanasema Stevo Simple Boy tafadhali chagua binti mmoja wetu awe mke wako. Nina uhakika sema sasa hivi sina bando ningewaonyesha. Wapo wengi,” alisema Stevo.

Msanii huyo alifichua kwamba mke wake wa sasa hivi ni raia wa Tanzania ambaye alimpata kwa njia hiyo hiyo ya kumvizia kwenye DM.

Akizungumzia vita vya kibabe katika muziki wa rap kwenye mataifa haya mawili, Stevo alisema;

“Marapa wa Tanzania mtuli, mtulize boli juu uwanja ni mdogo, sisi marapa wa Kenya tuko na uwezo mwingi kuwaliko.”

Stevo alisema kuwa wanadada wengi wanampenda kwa kile alisema kuwa yeye ni wa moto asiyeweza kuepukika.

“Wanadada wenyewe tu ndio wananipenda kwa sababu mimi ni mtanashati, niko wa moto na mimi ni mtamu. Wanavutiwa na muonekano wangu lakini pia mimi najilinda,” alisema.

“Wasichana wengi wananifuata wakitaka kufanya mapenzi na mimi, wanahisi wakifanya mapenzi na mtu maarufu kama mimi wanahisi vizuri,” aliongeza.