Nakupeza sana-Mwanawe Esther Musila amkumbuka baba yake kwa ujumbe mtamu

Mbali na Gilda, Esther Musila pia ana mtoto mwingine wa kiume anayeitwa Glen Naibei.

Muhtasari
  • Gilda alikiri kwamba kutokuwepo kwa baba yake kulihisiwa hadi sasa licha ya kwamba miaka mingi imepita.

Bintiye Esther Musila, Gilda Naibei leo ameandika ujumbe wa heshima kwa marehemu babake ambaye inasemekana aliaga dunia miaka saba iliyopita.

Gilda, ambaye pia ni mwanahabari wa mtindo wa maisha katika Standard Media Group alikumbuka nyakati walizokaa na babake na jinsi alivyokuwa mcheshi kabla ya kifo kisichotarajiwa.

Gilda alikiri kwamba kutokuwepo kwa baba yake kulihisiwa hadi sasa licha ya kwamba miaka mingi imepita.

Mwanahabari huyo alifikiria zaidi jinsi baba yake angejivunia yeye na kazi yake ya uandishi wa habari kutokana na ukweli kwamba alikuwa mpenzi wa magazeti.

"Baba nimekukumbuka tu. Kukuona tu au kucheka na wewe. Ulikuwa unasoma magazeti kila siku hivyo najua ungejivunia kumuona binti yako." Gilda aliandika.

Familia hata hivyo ilipata faraja baada ya mwanamuziki Guardian Angel kuwa sehemu yao.

Guardian ndiye baba wa kambo wa Gilda Naibei baada ya kumuoa mamake Gilda Esther Musila.

Mbali na Gilda, Esther Musila pia ana mtoto mwingine wa kiume anayeitwa Glen Naibei.

Familia hiyo mara kwa mara imeshiriki video na picha zao wakiburudika kwenye mitandao ya kijamii, ishara ya kweli ya furaha yao mpya.

Pia alikumbuka jinsi binamu zake walisema wana mjomba mzuri ilhali wao ndio walikuwa na baba mzuri dunuiani.

Alimtaka aendelee kupumzika kwa amani.

"Wengi walidhani wewe ni mjomba mzuri lakini tulipaswa kuwa na baba mzuri. ulifanya maisha kuwa ya kawaida na ya kawaida. I miss that the most rest on dad."