'Taarifa yangu ilitolewa out of context,'Khaligraph Jones awaomba Watanzania msamaha

Rapa huyo aliwaambia Watanzania kwamba ujuzi wao wa kurap ulikuwa chini sana

Muhtasari
  • Katika mahojiano na Wasafi hivi karibuni, rappa huyo anasema kuwa kauli yake hiyo ilitolewa nje ya muktadha.
  • Alitishia kutwaa tasnia hiyo nchini Tanzania iwapo watashindwa kufanya lolote kuihusu
Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: Screengrab

Rapa Khaligraph Jones amekuwa akivuma mitandaoni tangu alipoamua kutoa changamoto ka wasanii wa Tanzania.

Kufuatia majibizano hayo makali, Khaligraph amemuomba msamaha kwa marapa.

Katika mahojiano na Wasafi hivi karibuni, rappa huyo anasema kuwa kauli yake hiyo ilitolewa nje ya muktadha.

“Blogger ni blogger. Blogger lazima atafute habari ambayo itaisha kabisa. In that aspect mazungumzo na mazungumzo yalikua yanaendelea, statement yangu imetolewa out of context kidogo. For the longest time, watanzania in terms of music we can never discredit the fact that music yenu imekuwa superior kidogo in general.

“Hata kwenye mimi mwenyewe niliona iyo interview venye imekatwa, sikuskia vizuri yaani, niliona imeniweka kwa picha mbaya nikasema ah, it wasn’t supposed to be like that because najua watu wengine hawatawai elewa yani ivo. That one I apologise for, that one I’m gonna apologize for that yaani hiyo haikuanga sawa hiyo unanipata? Kauli yangu ilitolewa muktadha,” alisema.

Rapa huyo aliwaambia Watanzania kwamba ujuzi wao wa kurap ulikuwa chini sana. Alitishia kutwaa tasnia hiyo nchini Tanzania iwapo watashindwa kufanya lolote kuihusu

“Rap wa TZ alikuwa amekufa isipokuwa Lunya, Mex na wengine wachache. Waliobaki wanafanya amapiano, record diss tracks before attack everyone na msnijibu na amapiano,24 hrs kama mnajiamini, ikishindikana nitakuja kufanya mashambulizi nije nichukue tasnia nzima ya rap Tanzania na nitakuwa bora. rapa nchini Tanzania kama nilivyo Kenya na Nigeria,” Khaligraph alisema.

Kauli hiyo ilivuta hisia kali kutoka kwa Watanzania, ambao hawakuacha kumshambulia kwa njia tofauti ikiwamo kuachia nyimbo za diss. Wakenya hata hivyo walisimama na Khaligraph na kuwapa changamoto zaidi rappers wa Tanzania.