Willy Paul amkejeli Bahati baada ya kutoa wimbo wa injili, 'Naskia Madem wamerudi gospel'

Pozee alidokeza kwamba baada ya Bahati kusikia anatoa albamu yake ya kufunga mwaka, ameamua kurudi kwenye injili, akimdunisha kama 'mrembo' kutokana na mavazi yake hivi karibuni.

Muhtasari

• Msanii huyo japo hakumtaja Bahati moja kwa moja, alimpiga kumbo akirejelea mtindo wake wa mavazi wa hivi karibuni.

Pozee amshambulia Bahati.
Pozee amshambulia Bahati.
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya humu nchini Willy Paul amemchokoza kwa mara nyingine tena aliyekuwa rafiki yake enzi za Sanaa yao ya kuimba injili, Bahati.

Pozee ambaye alitangaza kuwa yuko jikoni kuandaa alabamu yake ya kufunga mwaka alisema kwamba Bahati ameingiza baridi na ndio maana ameamua kurudi kwa injili – akirejelea msanii huyo wa EMB Records kuachia wimbo wake wa injili ‘Utarudi Lini?’ hivi majuzi.

Willy Paul ambaye amekuwa akilazimisha bifu na Bahati kwa miaka ya hivi karibuni tangu wote watoke kwenye injili na kuanza kutunga mashairi ya kidunia alisema kwamba wasanii washindani wake – akiwemo bahati – wameogopa kuhusu ujio wa albamu yake.

Msanii huyo japo hakumtaja Bahati moja kwa moja, alimpiga kumbo akirejelea mtindo wake wa mavazi wa hivi karibuni kuvaa kama mwanamke na kusema kwamba ‘mrembo ameamua kurudi kwa injili’.

“Albamu yangu ya Mwaka inashuka hivi karibuni, Wasanii Tayari Wameanza Uwoga Na Vitisho Baridi. Ninachowaletea Ni Album Halisi,” alisema msanii huyo mwenye mikogo kutoka lebo ya Saldido.

Naskia Kuna Wale Wataacha Muziki Na Madem Wengine Watarudi Gospel. Anyway Si Ni Life? POZZE Ameamua,” aliongeza.

Baada ya watu kadhaa kuanzisha kampeni ya kumrai Bahati kurudi kwenye muziki wa injili ambao aliuacha miaka kadhaa iliyopita baada ya kuoa, Bahati anaonekana kusikia ombi la mashabiki wake na siku mbili zilizopita aliachia kibao cha injili akiuliza Mungu ni lini atarudi.

Kabla ya kuachia kibao hicho, Bahati aliwaacha wengi kwenye utata baada ya kuweka picha ya jeneza na pembezoni mwake picha ya maombolezo ikionesha sura yake na kuandika kwenye kapsheni ‘Utarudi Lini’ ambapo wengi walimsuta kwa kutumia picha yake kwenye jeneza kuashiria kifo au mauti.