Jackie Matubia adokeza kwa nini ameridhika na maisha bila mchumba

Jackie alitengana na mchumba wake Blessing Lungaho miezi michache iliyopita.

Muhtasari

•Katika kanda ya video ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Tiktok, mama huyo wa watoto wawili alitoa taarifa kuhusu maisha yake.

•Haya yanajiri siku chache baada ya fununu kuenea kuwa ameonekana kwenye picha ya mpenzi wake wa zamani akimpokeza ua la waridi.

Image: INSTAGRAM/ JACKIE MUTUBIA

Muigizaji maarufu nchini Kenya Jackie Matubia amedokeza kuwa kwa sasa hawezi kulalamika kuhusu maisha kwani yanampeleka kulinganga na matarajio yake.

Katika kanda ya video ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Tiktok, mama huyo wa watoto wawili alitoa taarifa kuhusu maisha yake.

Alitumia sauti maarufu ya mtandao wa tiktok kusema kwamba hakuna anyemsisitiza kwani ana kila kinachoitajika kwa maisha.

"I got money, I`ve got a job, aint nobody cheating on me,"alisema.

Kumaanisha, "Nina pesa, nimepata kazi, hakuna anayenidanganya."

Jackie walitengana na mpenzi wake Blessing miezi michache iliyopita.

Haya yanajiri siku chache baada ya fununu kuenea kuwa ameonekana kwenye picha ya mpenzi wake wa zamani akimpokeza ua la waridi.

Blessing Lung`aho, alikuwa amechapisha picha akiwa na mwanamke aliyesimama nyuma yake, akiwa amemfunika macho kwa mikono yake , jambo ambalo lilipelekea mashabiki wake kudhania kwamba wamepata kurudiana,

Aidha picha hiyo ya ya Blessing iliambatana na maandishi ya kutania kimapenzi, alisema;"

Allisema 'love is blind' lakini mimi niliona perfect match wangu pale *HelloMrRightke.Sasa Saturday night itakuwa nganga...and chill,me and my lady tukiwatch @drofweneke na @diana_bahati wakisaidia more ladies wapate Mr.Right."

Baada ya uvumi keunea kwamba mwanadada huyo alikuwa Jackie, muigizaji huyo alionekana mtandaoni akionyesha urembo wa mikono yake ili kuepusha uvumi huo kuenea kwamba alikuwa amerudiana na blessings.

"Je, unaweza kulinganisha makucha haya na yale, tafathali? sijiusishi ma maudhui mabaya. Gai,ata maua ya shilingi mia tatu haiwezi kununuliwa ili kufanya maudhui tu, wanachukua ya vase. Nikomeni," Alisema.

Jackie vile vile, amechapisha kanda nyingine kwenye tiktok, akiwaonya wale wanaotaka kumchumbia kuwa lazima wawe na pesa na wenye kutoa pesa zao.

"I rebuke the spirit of being admired by stingy men, Amen.""Nakemea roho ya kusifiwa na mwanaume wabahili, Amina."