Kelechi Africana adai ametunga mimba 22, lakini watoto anaowajua ni 13

Msanii huyo wa Mombasa alidai kwamba watoto wengine 9 hawajui kwa vile mama zao hawakutaka kumhusisha katika malezi bali walichokuwa na haja nacho kutoka kwake ni mbegu tu!

Muhtasari

• Mwimbaji huyo alisisitiza kwamba wasanii wote wa Muziki wa 001 bado wangefanya vyema ikiwa kweli walikuwa na talanta, kwa pesa za Joho au bila.

Kelechi Africana
Kelechi Africana
Image: Facebook

Rais wa kujitangaza wa muziki wa kizazi kipya katika ukanda wa Pwani ya Kenya Kelechi Africana amezua gumzo mitandaoni miongoni mwa mashabiki wake baada ya kudai wazi wazi kwamba yeye ni baba wa watoto 22.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Africana aliandika kwamba anachokijua au tuseme kukikumbuka ni kwamba ameshatunga mimba 22, lakini watoto ambao anawajua ni 13 tu, akidai kwamba hao wengine 9 hawajui kwa vile mama zao hawakutaka kumhusisha katika malezi kwani walichokuwa wanakitaka kutoka kwake ni mbegu tu na kibarua cha kulea ni kwao wenyewe bila kumhusisha.

Nina watoto 22 — ninao wajua ni 13 — hao wengine mama zao walitaka mbegu tu,” aliandika.

Msanii huyo ambaye amepoa kwa siku za hivi karibuni haswa baada ya kukamilika kwa hatamu mbili za uongozi wa aliyekuwa gavana wa Mombasa Hassan Joho hivi majuzi katika mahojiano katika kituo kimoja cha redio humu nchini alidai kwamba Sanaa ya muziki wa kisasa Pwani imedidimia kwani Joho ndiye alikuwa anawapa shavu wasanii wengi kuinukia.

Mwimbaji huyo alisisitiza kwamba wasanii wote wa Muziki wa 001 bado wangefanya vyema ikiwa kweli walikuwa na talanta, kwa pesa za Joho au bila.

"Jambo moja kuhusu wasanii wote ambao wamesukumwa hawajui jinsi ya kuimba. Wote, haswa uliowataja hawana talanta kweli. Lakini Joho bado yuko na bado ni tajiri, kwa hivyo swali ni, kwa nini wameacha kuachia nyimbo na kushamiri? Hiyo inakuonyesha wao si wazuri katika kile wanachofanya,” Kelechi Africana alisema.