Fahamu ni kwa nini Karen Nyamu amewaomba mashabiki wake msahama

Seneta Nyamu katika kipindi cha miaka kama mitatu iliyopita amekuwa akizungumziwa mitandaoni kuhusu mgogoro wa mapenzi unamhusisha na msanii Samidoh na mkewe wa kwanza Edday Nderitu.

Muhtasari

โ€ข Seneta huyo alisema haya akiwa katika ziara jijini Dubai katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harmad.

Karen Nyamu.
Karen Nyamu.
Image: Instagram

Seneta maalum Karen Nyamu amewataka mashabiki wake kumsamehe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku mbili zilizopita, Nyamu ambaye amekuwa akigonga vichwa vya habari kisa mgogoro wa kimapenzi baina yake na mke wa msanii Samidoh, Edday Nderitu kuhusu mapenzi ya msanii huyo alikiri kwa mashabiki wake kwamba ana moyo laini japo pia ana mdomo mchafu.

Seneta huyo alisema haya akiwa katika ziara jijini Dubai katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harmad.

Alipakia picha yake akiwa amesimama kwenye stairs na kukiri kwamba ana moyo laini lakini pia mdomo wake ni mchafu โ€“ labda kutokana na maneno ambayo hujatoa kwa kuwajibu watu mbali mbali bila kupepesa jicho.

โ€œUkiwa na moyo laini, lakini uwe na mdomo mchafu zaidi๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„ Aki mnisamehe ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ˜Œโ€ Nyamu aliandika.

Hata hivyo, mashabiki wake walimwambia kuwa hakuna haja ya kuwaomba msamaha kwa tabia yake wakisema kuwa wengi wao waliamua kumfuata na kumpenda jinsi alivyo.

Wengine walimwambia vimbwanga vyake vya kuwajibu shombo watu ndivyo vinawavutia kwake.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake;

โ€œTunakupenda vivyo hivyo โค๏ธโค๏ธ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅโ€ Brandon Rugi alimwambia.

โ€œYaaaani wewe mkenya nakupendaga sana karbu Tanzania,โ€ Kaiza Andrea aliwmabia.

โ€œKumbe ulienda kuwakilishs Harambee stars,โ€ Nancy Kwamboka alisema.

Seneta Nyamu katika kipindi cha miaka kama mitatu iliyopita amekuwa akizungumziwa mitandaoni kuhusu mgogoro wa mapenzi unamhusisha na msanii Samidoh na mkewe wa kwanza Edday Nderitu.

Hata hivyo, Nderitu alionekana kukata tamaa na huba la Samidoh na kufunga virango kabla ya kutokomea zake Marekani.

Akiwa Marekani, aliweka wazi sababu zilizomfanya kuondoka katika ndoa aliyokuwa ameikuza kwa miaka 15, sababu kuu akiitaja kuwa ni wanawe ambao alilenga kuwalinda kisaikolojia kutokana na ukakasi unaoendelea  baina yake ya Karen Nyamu.