Eric Omondi afichua sababu ya kuacha kazi Radio Jambo baada ya miezi 8 tu!

Mchekeshaji huyo alikiri kwamba alikuwa anafika studioni asubuhi akiwa amelemewa na usingizi kwani usiku uliopita alikuwa anafanya shoo katika vilabu mbalimbali.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo alikiri kwamba kulikuwa na mgongano baina ya kuweka sawa kazi mbili katika ucheshi na redioni.

Eric Omondi ata gaza nia ya kujiingiza katika siasa.
SIASA Eric Omondi ata gaza nia ya kujiingiza katika siasa.
Image: Facebook

Mchekeshaji Eric Omondi kwa mara ya kwanza amezungumzia ni kwa nini aliondoka katika stesheni ya Radio Jambo baada ya kufanya kazi ndani ya miezi minane tu.

Akizungumza na mchekeshaji mwenzake Oga Obinna katika chaneli yake ya YouTube, Omondi alikiri kwamba hakufukuzwa redioni bali alilemewa kutokana na kazi.

“Nilikuwa Radio Jambo, na katika ukuaji wa mtu mimi nilikuwa katika kilele cha taaluma yangu. Kwa hiyo mimi si mtu wa asubuhi, lakini nakumbuka nilikuwa hapo na Gidi na Ghost. Nikafanya Jambo kwa miezi minane nikalemewa. Mimi na meneja wangu tukakubali tukajiambia ukweli kwamba kufanya katika redio hakuendani na mimi,” Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo alikiri kwamba kulikuwa na mgongano baina ya kuweka sawa kazi mbili katika ucheshi na redioni na kwa wakati mmoja ilimbidi kukosa shoo mbili kubwa zilizokuwa zimuingizie takribani nusu milioni kwa sababu tu alikuwa anahitajika kuwa katika redio.

“Kuna shoo mbili tulikosa za Barclays za Kisumu, zilikuwa kama nusu milioni na hivyo ndivyo tuliamua kuandika barua kwa uongozi,” alisema.

Baada ya kuona kuwa analemewa na kazi redioni, Omondi alisema kwamab ilimbidi ashauriane na meneja wake na waliandika barua ya kuacha kazi.

Baadae alijiingiza katika ziara ya duniani kwa ucheshi ambapo mpaka sasa Marekani ametembelea majibmo 17.