Kanye West ashtakiwa kwa kukataa nyumba yake isiwe na madirisha, maji na umeme

Kanye alimfuta kazi meneja aliyekuwa anasimamia ujenzi wa jumba lake la kifahari baada ya kukataa kutii agizo lake kwamba nyumba isiwe na madirisha, umeme wala maji.

Muhtasari

• Kulingana na kesi hiyo, mjasiriamali huyo wa Yeezy anadaiwa kuamuru Saxon, 32, kupeleka jenereta kubwa ndani ya nyumba hiyo.

Kanye West
Kanye West
Image: BBC NEWS

Rapa mwenye utata kutoka Marekani, Kanye West anakabiliwa na kesi nyingine baada ya kumfuta aliyekuwa anasimamia mradi wa ujenzi wa jumba lake la kifahari.

Kwa mujibu wa jarida la Independent UK, Kanye West alimfuta msimamizi wa mradi huo kazi baada ya kukataa kutii agizo la Kanye West kwamba nyumba yake isiwekwe maji, madirisha wala umeme.

“Tony Saxon alidaiwa kufukuzwa kazi baada ya kukataa "kuzingatia" na kuondoa umeme na madirisha kutoka kwa nyumba ya Ye's Malibu ili kuunda makazi ya mabomu ya retro,” kituo cha runinga cha NBC News iliripoti.

 Kulingana na NBC News, kesi iliwasilishwa Jumatano katika Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Los Angeles.

Kesi ya meneja wa mradi inadai ukiukaji wa kanuni nyingi za kazi, ikiwa ni pamoja na mazingira hatari ya kufanya kazi, mishahara isiyolipwa, na kukomesha kulipiza kisasi kimakosa.

Kulingana na kesi hiyo, mjasiriamali huyo wa Yeezy anadaiwa kuamuru Saxon, 32, kupeleka jenereta kubwa ndani ya nyumba hiyo.

Lakini meneja wa mradi alipokataa, Kanye West alimwambia "kutoa upuuzi wake hapa". Rapa huyo pia aliripotiwa kusema kwamba Saxon "atachukuliwa kuwa adui ikiwa hatafuata alichokua anataka".

Baada ya kumfanyia kazi rapper huyo kwa muda wa miezi miwili, West aliripotiwa kumfukuza kazi Saxon tarehe 5 Novemba 2021 kwa kutotii maombi hayo.

Rapa huyo pia anadaiwa kuahidi kulipa Saxon $20,000 kwa wiki. Hata hivyo, kulingana na kesi hiyo, West alifanya malipo mawili pekee: moja ili kufidia mshahara wa kila wiki wa Saxon na nyingine kwa bajeti ya mradi.