'Punguzeni mabati kwa shingo,'Otile Brown awachana Diamond na Mbosso kwa kuvaa cheni feki

Kulingana na yeye, wanachovaa hudumu kwa miezi michache tu kwani hupata kutu kwa urahisi.

Muhtasari
  • Shambulio la Otile dhidi kwa waimbaji wa bongo fleva linakuja mwaka mmoja baada ya kukutana na rapa Lil Baby kwenye Icebox, alipokuwa akinunua vito.

Mwimbaji Otile Brown amewachana wasanii wa Tanzania Diamond Platnumz na Mbosso kwa kuvaa vito vya bandia.

Hii ni baada ya wawili hao kuonekana wakijaribu ubora wa vito vyao kwenye video ambayo ilisambazwa kwenye akaunti ya Instagram ya Mbosso.

Akitumia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Otile Brown aliwakashifu akiwataka wapunguze kuvaa mabati au maarufu zaidi kama karatasi za chuma kwa Kiingereza.

Kulingana na yeye, wanachovaa hudumu kwa miezi michache tu kwani hupata kutu kwa urahisi.

“Kwa upendo, punguzeni mabati kwenye shingo au weka kabisa, mnachoresha…hao ni watu gani mnanunua chain kwao? Tuelewane. Utakuwa unaongea tajiri kila wakati na bado unatingisha fungazi. Inspire game ujanja ujanja wa nini and y’all are blessed chain baada ya miezi kadhaa huoni imeshika kutu,” alisema.

Aliendelea kupendekeza maduka halali ya vito kama; vito bila kikomo, Ice Box, Johnny dang na sonara A.

Shambulio la Otile dhidi kwa waimbaji wa bongo fleva linakuja mwaka mmoja baada ya kukutana na rapa Lil Baby kwenye Icebox, alipokuwa akinunua vito.

Alijipatia kishaufu kilichopakwa almasi na picha ya marehemu bibi yake.

Huku akionyesha mkufu huo Mbosso aliwaonya wasanii wenzake dhidi ya kuvalia cheni feki.