Mrembo mwenye pua kubwa alia kwa uchungu baada ya kila mwanamume kumkakaa - video

Alikuwa anajibu kwa mtumizi mmoja wa mtandao huo aliyemuuliza iwapo yuko na mpenzi wa kiume.Alianza kutiririkwa na machozi akisema kwamba anatumai angekuwapo na mpenzi hata mmoja lakini kwa bahati mbaya hana

Muhtasari

• “Natamani ningekuwa na mmoja,” alijibu huku nyuma akiweka wimbo uliokuwa unaimba kwa kumfariji.

Mrembo mwenye pua kubwa
Mrembo mwenye pua kubwa
Image: Tiktok

Mrembo aliye na pua kubwa lisilo la kawaida amechukua masikitiko yake katika mtandao wa video fupi wa TikTok kuonesha huzuni yake kwa kukataliwa na kila mwanamume.

Mrembo huyo alidokeza kwamba pengine kila mwanamume anamkataa kwa kumuona kuwa si mrembo kutokana na ukubwa na unene wa pua lake.

Katika video ambayo mrembo huyo alipakia kwenye uurasa wake wa TikTok @AmmieSweeshy, alikuwa anajibu kwa mtumizi mmoja wa mtandao huo aliyemuuliza iwapo yuko na mpenzi wa kiume.

Alianza kutiririkwa na machozi akisema kwamba anatumai angekuwapo na mpenzi hata mmoja lakini kwa bahati mbaya hana hata huyo mmoja wa kumtamani.

“Natamani ningekuwa na mmoja,” alijibu huku nyuma akiweka wimbo uliokuwa unaimba kwa kumfariji.

“Mbona nina hisia sana? Hapana, sio sura nzuri, pata kujidhibiti. Na ndani kabisa najua hii haifanyi kazi kamwe. Lakini unaweza kulala nami ili isiumie,” wimbo huo wa Sam Smith – Stay with me – uliimba kwa kumfariji huku akishindwa kuzuia mifereji ya machozi machoni.

Baadhi ya watu walisimama upande wa faraja yake huku wengine wakimtania kutokana na pua lake kubwa na hata wengine kudai kwamba huenda si pua la kweli bali ametulia program za kuhariri muonekano wa mwili wa binadamu kwenye simu.

“hey tafadhali nifollow back😅Nina pua kubwa kama wewe” AB Studios.

“unalia kwa sababu huwezi kuwa na mwanaume 😭 fanya bidii uwe na pesa rekebisha hiyo pua na uwe msichana mjanja,” mwingine alimwambia.

“Wewe ni mrembo sana, usiruhusu kile wanachosema watu kiharibike, mimi niko single Ikitokea unahitaji mpenzi lemme know,” mwingine alimwambia.