Tamasha la msanii Burna Boy limeghairiwa kutokana na mauzo ya chini ya tiketi

Tamasha la moja kwa moja la Burna lilipangwa kufanyika Septemba 23, kwenye Uwanja wa FNB mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Muhtasari

•Kauli ya Burna inakuja baada ya kampuni ya Tiketi, Ticket Pro, kutangaza Jumatano kwamba onyesho hilo lililotarajiwa sana, linaahirishwa kwa sababu ya "ukosefu wa tikiti" ya mauzo, kati ya sababu zingine.

Burna Boy/Instagram
Burna Boy/Instagram

Msanii wa Nigeria Damini Ogulu, almaarufu Burna Boy, ameghairi tamasha lake la moja kwa moja lililokuwa likitarajiwa nchini Afrika Kusini kutokana na kile ambacho timu yake ilidai kuwa mapromota hao 'kutoweza kutimiza wajibu wao wa kimkataba.

Tamasha la moja kwa moja la Burna lilipangwa kufanyika Septemba 23, kwenye Uwanja wa FNB mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Kauli ya Burna inakuja baada ya kampuni ya Tiketi, Ticket Pro, kutangaza Jumatano kwamba onyesho hilo lililotarajiwa sana, linaahirishwa kwa sababu ya "ukosefu wa tikiti" ya mauzo, kati ya sababu zingine.

"Tunasikitika kutangaza kuahirishwa kwa tamasha la Burna Boy lililokuwa likitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa FNB, Johannesburg tarehe 23 Septemba 2023," taarifa kutoka kwa Ticket Pro ilianza.

Tamasha hilo sasa litafanyika tarehe 16 Desemba 2023.

“Uamuzi huu haukufanywa kirahisi na promota na umekuja kutokana na kuzingatiwa kwa kina na tathmini ya mambo mbalimbali, ikiwamo kukosekana kwa mauzo ya tiketi.

Hata hivyo, Usimamizi wa Spaceship, kampuni ya usimamizi ya Burna’s Boy, tangu wakati huo imejibu madai haya ya Ticket Pro, ikisema kushindwa kwa waendelezaji wa tamasha la Ternary Media Group kutimiza majukumu yao ya kifedha, uzalishaji na kiufundi kwa timu.

"Cha kusikitisha, ni kwa masikitiko makubwa kwamba lazima tuwajulishe kwamba licha ya juhudi za timu yangu, onyesho la Johannesburg mnamo Septemba 23, litakatishwa kwa sababu ya mapromota kushindwa kutimiza majukumu yao ya kimkataba, kifedha, uzalishaji na kiufundi.Wachuuzi wa uzalishaji bado hawajalipwa na kwa hivyo, ni dhahiri katika hatua hii kwamba kiwango cha uzalishaji kilichokubaliwa kinachohitajika kwa ukubwa huu wa ukumbi hakiwezi kufikiwa,"

Spaceship iliomba radhi kwa mashabiki wake na kuwaimiza kusalia kuwa wavumilivu

"Tunaeleza kwamba kampuni zote za tikiti lazima zihakikishe kwamba zinarejeshwa kikamilifu.Poleni sana mashabiki wote, tunatarajia kuwaona nyote hivi karibuni."

Kufikia wakati habari hizo zilipoibuka, Awamu ya 1 pekee ya mauzo ya tikiti ndiyo ilikuwa imefikia uwezo wake. Gharama hizi ni kati ya R765 hadi R1,510 (takriban Ksh 11,000)

Tikiti za awamu ya 2 ambazo bado zinapatikana ni kati ya bei kutoka R950 hadi R2,660 (takriban Ksh.20,000).

Nyota huyo wa Nigeria alipewa kadi ya kujaza Uwanja wa FNB wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 90,000, akitoka kuuza Uwanja wa London Stadium wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 na hivi majuzi Uwanja wa Citi Field wenye viti 41,800 huko Queens, NY.

Onyesho lake la mwisho nchini Afrika Kusini lilikuwa mwaka wa 2022, ambapo aliongoza tamasha la DStv Delicious.