Khaligraph amjibu mrembo aliyemtamani kimapenzi na kusifia mwili wake wa sixpack

Khaligraph alimpiga rafiki yake Breeder LW through pass safi kumchukua mrembo huyo ili kuwa mpenzi wake, akisema kwamba yeye ameshaoa.

Muhtasari

• Hitmaker huyo wa Yego alikuwa amevalia koti jeupe na suruali na viatu vinavyoendana.

• “Huwezi shinda hio race bro acha kushindana na watu ambao hawashindani na wewe. Utapoteza. Heshimu OG,” alisema.

Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: Insta

Msanii namba moja wa rap nchini Khaligraph Jones amemjibu shabiki wa kike ambaye alionesha kumtamani kimapenzi huku akimezea mate mwili wake uliochongenga vizuri kwa mapande sita.

Siku ya Alhamisi, rapa huyo nguli alishiriki picha yake na mtu asiyejulikana katika eneo lililoonekana kuwa la kuegesha magari.

Kwenye kapsheni ya picha hiyo, Jones aliwataka watu kutoshindana na watu ambao hawawajui lakini kwa upande wa kuandika maoni, warembo walimwagika na kuonesha jinsi ambavyo wanatamani kumegewa japo kidogo penzi la msanii huyo.

Hitmaker huyo wa Yego alikuwa amevalia koti jeupe na suruali na viatu vinavyoendana.

“Huwezi shinda hio race bro acha kushindana na watu ambao hawashindani na wewe. Utapoteza. Heshimu OG,” alisema.

Mrembo mmoja kwa jina Original Rahma alishindwa kuficha tamaa zake na kumuandikia kwamba huwa anahisi mchecheto pindi anapomuona Khaligraph haswa kwa mwili wake uliositunya na kujaziana kwa kiasi cha haja.

“Jamani Khali unaniumiza na mwili huo,” alikiri mrembo Rahma.

Hata hivyo, Khaligraph alimjibu kwa ukarimu akimwambia kwamba tayari yeye ameshaoa na kutoka soko.

Alimuuliza kama atakubali amsukume kwa rafiki yake, msanii Breeder LW ambaye awali tuliripoti kwamba alikiri ndoto yake ni kuoa wanawake 200.

“@original__rahma wacha nikupee jamaa anaitwa @breeder_lw size yako huyo, Mimi nishaoa tayari,” Khaligraph alimjibu.

Katika mahojiano hayo ya awali ambayo Radiojambo.co.ke iliripoti, Breeder alisema kwamba yeye bado hajaoa lakini ana wapenzi wa kike kutoka angalau kila eneobunge na kila mtaa wa jiji.