Ukiona nikijenga nyumba ya 10m jua kuna 10m zingine kwa akiba - Mulamwah

“Mimi sioni kama ni mapema sababu sioni kama ni mapema kwa sababu mimi sihisi hilo shinikizo na mzigo wa kujenga, mpaka sasa imekula kama milioni 10 na bado milioni 4 ndio ikamilike, na hizi ni pesa kidogo,” Mulamwah.

Muhtasari

• "Ukiniona nimejenga kwa shilingi milioni 10 wewe jua tu niko na milioni 10 nyingine, kwa hiyo si eti pesa zimeishia huko, kuna zingine,” aliongeza.

• Mulamwah anasema haya ikiwa ni wiki mbili baada ya Wakenya mitandaoni kuzua kwamba kujenga nyumbani ni kutupa pesa.

azunguzia maendeleo ya ujenzi wa jumba lake la kifahari.
Mulamwah azunguzia maendeleo ya ujenzi wa jumba lake la kifahari.
Image: Facebook

Mchekeshaji Mulamwah hatimaye amevunja kimya chake kuhusu watu wanaomkosoa kwa kuwekeza mradi mkubwa wa ujenzi wa jumba lake la kifahari kijijini mwao hali ya kuwa asilimia kubwa ya maisha yake anaishi mjini.

Akizungumza katika kipindi cha The Wicked Edition ndani ya runinga ya NTV, Mulamwah alisema kwamba alipoanza kujenga, alipata watu wengi ambao wanamkosoa kwa kujenga hali ya kuwa bado ni kijana mdogo lakini akasema kwamba wao ndio wanaona inamwia vigumu lakini kwake anachokifanya ni kununua uhuru wake wa kifedha mapema.

“Mimi sioni kama ni mapema sababu sioni kama ni mapema kwa sababu mimi sihisi hilo shinikizo na mzigo wa kujenga, mpaka sasa imekula kama milioni 10 na bado milioni 4 ndio ikamilike, na hizi ni pesa kidogo,” Mulamwah alisema.

“Mimi sioni kama ni vibaya kwa sababu hiyo ni njia moja ya kununua uhuru wangu wa kifehda kwa sababu hapa mbele sitakuwa na’save pesa. Nitakuwa na save ya nini wakati nimeshajenga?”

“Mimi naamini ukipata nafasi ya kujenga wewe jenga tu, maana ni kitu ambacho kinaingia kwa moyo na unafanya pole pole bila presha. Mimi sioni ni mapema kujenga. Ukiniona nimejenga kwa shilingi milioni 10 wewe jua tu niko na milioni 10 nyingine, kwa hiyo si eti pesa zimeishia huko, kuna zingine,” aliongeza.

Mulamwah anasema haya ikiwa ni wiki mbili baada ya Wakenya mitandaoni kuzua kwamba kujenga nyumbani ni kutupa pesa.

GAumzo hilo limevutia maoni kutoka pande mbili na lilianzishwa na Obinna ambaye kwa upande wake alisema haoni kama ni vizuri kwa Mulamwah kuwekeza pesa nyingi kijijini hali ya kuwa maisha yake mengi kabla ya kustaafu atayatumikia mjini.