Watu wananihukumu kwa sababu nilifanya kazi kwenye televisheni- Kimani Mbugua

Mbugua amesema kwamba amekuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo.

Muhtasari

•Mbugua amesema kwamba watu wengi wanamuhukumu baada ya kutangaza  kupitia video aliyochapisha kwenye Instagramu kwamba anapitia hali ngumu ya kujikimu kimaisha.

•"Tayari kufikia sasa tumekusanya pesa zaidi ya nilivyokuwa natarajia. Na singepata pesa hizo kama sio kuzungumzia shida yangu," alisema.

Kimani Mbugua/Instagram
Kimani Mbugua/Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa televisheni Kimani Mbugua ameeleza masaibu anayopitia kwa sasa baada ya kupoteza kazi yake mwaka wa 2020.

Katika mahojiano, Mbugua alisema kwamba watu wengi wanamuhukumu baada ya kutangaza  kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba anapitia hali ngumu ya kujikimu kimaisha.

Alieleza kwamba yeye kufanya kazi na Runinga ya Citizen hapo awali, inapelekea watu kutomuamini wakati ambapo anaomba masaada.

"Kufanya kazi kwa televisheni, si kwamba unapokea mamilioni,kile ambacho unalipwa unapata unapata majukumu ni makubwa zaidi." Alisema kwenye mahojiano na Oga Obinna.

Mwanahabari huyo alieleza kwamba aliathirika kiafya kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya. Hilo lilimpelekeka yeye kujiuzuru kutoka kazini baada ya kugundua kuwa hali yake imedhoofika mwaka wa 2020.

Aliendelea kusema kwamba, alichukua hatua hiyo ya kufichua hali yake kwa umma kwani msaada aliohitaji, hakuna mtu binafsi ambaye angefanikisha, akisema kufikia sasa amepokea msaada mkubwa kutoka kwa watu wenye nia nzuri.

"Tayari kufikia sasa tumekusanya pesa zaidi ya nilivyokuwa natarajia. Na singepata pesa hizo kama sio kuzungumzia shida yangu." Aliongeza.

Kulingana na maelezo yake, amekuwa akihudumiwa kiafya kwa muda wa mwaka mmoja, suala ambalo anasema lilimtenganisha na watu kwa muda huo wote.

Amesema kwamba amekuwa akisumbuliwa na  hali ya msongo wa mawazo.

Mbugua pia ameeleza masaibu aliyopitia usiku huo baada ya kuchapisha video hiyo,akisema kwamba alikosa nauli za kuenda nyumbani hivyo kumpelekea kulala kwenye mitaro.

Aidha anasema alikosa mtu wa kuomba simu, ili kutumia kuomba angalau  nauli.

Obinna, alimpongeza kwa maamuzi aliyochukua kusimulia hali yake akisema ni wengi hasa vijana wa kiuma ambao wanapitua hali ngumu kama ya Mbugua ila hawazungumzi kupata usaidizi.