kipusa aliyemkataa ombi la Bahati alimsaindia kumpata Diana Marua

Diana alikuwa mfuasi wangu mkubwa na wakati huo alikuwa msanii aliyejulikana kwa utunzi wa nyimbo.

Muhtasari

• Familia ya Bahati imebarikiwa watoto watano; Morgan, Mueni, Heaven, Majesty na Malaika.

• Licha ya kuwa baadhi ya watoto ni wa kupanga Bahati anaisha nao kwa mapenzi tele kama watoto wake.

Diana Marua na Bahati.
Diana Marua na Bahati.
Image: Instagram

Mwanamuziki Kelvin Kioko maarufu Bahati amefunguka kupitia Instagram jinsi alikutana na mke wake ambaye pia ni msanii Diana Marua.

Haya yanajiri  siku chache baada ya mahojiano ya moja kwa moja  yaliofanyiwa msanii Bahati akitaja tarehe 20 mwezi oktoba kuwa siku yake muhimu kusherekea miaka saba katika ndoa na kuahidi kumtunuku mkewe zawadi saba kuadhimisha miaka saba ya ndoa.

"Nilikuwa nimeandika wimbo wangu  wa injili ,mwanadada  niliyetaka  kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu sikufua dafu kumfikia alikataa ombi langu", alisema Bahati.

Bahati amesimulia baada ya kukosa huduma za mtangazaji huyo alimtumia ujumbe Diana Marua ambaye alikuwa mfuasi wake kwenye mitandao ya kijamii licha ya kwamba walikuwa hawajawahi kukutana ana kwa ana. 

Diana alikuwa mfuasi wangu mkubwa na wakati huo alikuwa msanii aliyejulikana kwa utunzi wa nyimbo na ushirikisho wa video nilipomuomba ombi alikubali na tukaanza urafiki na hapo safari yetu ya mapenzi ikaanza. 

"Mungu alimtumia mwanadada huyo wa Runinga kukataa ombi langu ndiposa nilikutana na kipenzi changu cha roho Mungu ni mwaminifu ametuweka pamoja mpaka sasa tunaadhimisha miaka saba ndani ya ndoa ,alisema.

Familia ya Bahati imebarikiwa watoto watano; Morgan, Mueni, Heaven, Majesty na Malaika Bahati licha ya kuwa baadhi ya watoto ni wa kupanga Bahati anaisha nao vizuri kama watoto wake.