Pete yangu ya harusi nilinunua kwa shilingi 15 - Pasta Ezekiel

“Lakini nilivalishwa pete ya kiroho ambayo imefanya ndoa yangu kuwa hai mpaka leo. Na hiyo pete ya kiroho ni bei ghali asikuambie mtu,” Ezekiel alisema.

Muhtasari

• Mchungaji huyo hata hivyo alisema kwamba kabla ya kuvishwa pete hiyo, Mungu alimvisha pete ya kiroho ambayo ameitaja kuwa ya bei ghali Zaidi.

Image: The star

Mchungaji mwenye utata kutoka kanisa la New Life Prayer Centre huko Mavueni kaunti ya Kilifi, Ezekiel Odero ameashiria kwamba pete za bei ghal ipasi na upako wa Mungu ndani ya ndoa huyo ndicho chanzo kikubwa cha kusambaratika kwa ndoa nyingi siku hizi.

Ezekiel ambaye alikuwa anahubiri katika kanisa lake na kumuuliza mwanamke mmoja aliyekwenda kutafuta nyota ya kurudisha ndoa yake iliyosambaratika alimuuliza bei ya pete yake na kulinganisha na pete yenye alifanyia harusi yake na mkewe Sarah.

Mchungaji huyo mwenye mahubiri ya utata alisema kwamba yeye alinunua pete ya shilingi 15 tu pesa za Kenya na ndoa yake imedumu hadi leo hii lakini muumini huyo alikuwa amenunua pete yake kwa Zaidi ya elfu 18 na haikuweza kudumu kwa miaka mingi.

“Pete ya harusi yangu hii mnaona nilinunua shilingi 15,” Ezekiel alisema.

Mchungaji huyo hata hivyo alisema kwamba kabla ya kuvishwa pete hiyo, Mungu alimvisha pete ya kiroho ambayo ameitaja kuwa ya bei ghali Zaidi.

“Lakini nilivalishwa pete ya kiroho ambayo imefanya ndoa yangu kuwa hai mpaka leo. Na hiyo pete ya kiroho ni bei ghali asikuambie mtu,” Ezekiel alisema.

Aliwashauri watu ambao wanataka kuenda kwenye ndoa kujitoa kwanza kwa Mungu kabla ya kuingia kwenye ndoa, pia akijitapa kwamba kanisa lake ndilo lenye upako wa kipekee wa kupatiana nyota ya ndoa.

“Kuna watu wanafurahi kwamba wanafanya harusi na pete ghali, nyinyi cheka. Lakini ukiolewa njoo New Life, la sivyo vile umeolewa na raha unaweza kuachwa hivyo hivyo, sababu harusi ni tukio, keki ni ya waliokuja harusi, chakula ni cha wambeya lakini ukifika kwa nyumba yako hivi, ndio ndoa inaanza,” alishauri.