'Wameanza kufanana', Mashabiki wasema Karen Nyamu akipakia video wakiwa na Samidoh

“Jamani nisikilizeni, mnisikilizeni, kuna wanawake warembo wenye marasa na mapaja na weupe na ni wazuri kinyama…” Samidoh aliimba sehemu ya mistari ya Longombaz.

Muhtasari

• Akiwa mwenye furaha na bashasha, Samidoh alikuwa akimuimbia Karen Nyamu wimbo wa TBT wa kundi la Longombaz, Vuta Pumzi

Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Image: Maktaba

Seneta mteule Karen Nyamu si wa kuficha tena mapenzi yake kwa baba wa watoto wake Samidoh, kwani amekuwa akipakia picha na video za pamoja wakipunja maisha kwa kijiko kikubwa cha dhahabu.

Jumatano jioni, Nyamu alipakia video kwenye isntagram story yake wakiwa wanajivinjari maisha ya Samidoh kwenye chombo kimoja huku Nyamu akiwa ndiye anarekodi video hiyo na Samidoh anamuimbia kwa kumdekeza na kumkaribia kama anataka kumlalia kwenye bega lake la kushoto.

Akiwa mwenye furaha na bashasha, Samidoh alikuwa akimuimbia Karen Nyamu wimbo wa TBT wa kundi la Longombaz, Vuta Pumzi;

“Jamani nisikilizeni, mnisikilizeni, kuna wanawake warembo wenye marasa na mapaja na weupe na ni wazuri kinyama…” Samidoh aliimba sehemu ya mistari ya Longombaz huku Nyamu akivaa sura ya haya na kujidekeza machoni pa baba watoto.

Hata hivyo baadhi ya Wakenya walihisi kwamba penzi la wawili hao limekolea kiasi kwamba wamefikia hatua ya kufanana.

“Ghai mpaka wameanza kufanana wallahi,” mmoja alisema.

“Hawa were meant for each other, love wins” Christine Anyango alisema.

“Choose what makes you happy..Love wins always” Philipa Ngila.

Nyamu na mpenzi wake wanaonekana pamoja siku chache baada ya kuweka wazi kwamba yeye kutoka kimapenzi na Samidoh licha ya kujua kwamba ana mke tayari – Edday Nderitu wala hajavunja sheria.

Seneta huyo alisema hayo wakati wa mahojiano kwenye runinga ya NTV ambapo alisema kwamba suala la mwanamume kuoa wanawake Zaidi ya mmoja liko kwenye katiba na yeye hajavunja sheria.