"Simwoni akivutia tena" Mrembo amtema Jamaa aliyemfadhili masomo chuo kikuu

Sasa katika mwaka wake wa mwisho, alisema haoni tena mvuto kwa sababu jamaa huyo anamkera na haonekani kuendana naye hata kidogo.

Muhtasari

• Katika ujumbe huo, mwanamke huyo alithibitisha kwamba mpenzi wake alimfundisha shuleni kuanzia mwaka wa kwanza hadi kumaliza masomo yake ya chuoni.

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Image: THE STAR, MOSES SAGWE

Mwanamke mmoja ambaye anakaribia kuwa mhitimu wa chuo kikuu amezua mjadala pevu katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter baada ya kudai kwamba amesalia katika njia panda kufanikisha lengo lake la kumtema jamaa aliyemfadhili masomo yake ya chuo kikuu.

Katika ujumbe huo, mwanamke huyo alithibitisha kwamba mpenzi wake alimfundisha shuleni kuanzia mwaka wa kwanza hadi kumaliza masomo yake ya chuoni.

Sasa katika mwaka wake wa mwisho, alisema haoni tena mvuto kwa sababu jamaa huyo anamkera na haonekani kuendana naye hata kidogo.

Aliongeza kuwa alipojaribu kumwambai jamaa huyo kwamba uhusiano wao hauwezi kuendelea tena kwa vle anamuona kama mwenye hadhi ya chini, jamaa wa watu anatishia kuachia picha zake za faragha iwapo atakataa ombi lake la ndoa.

“Mpenzi wangu alinifadhili masomo yangu kuanzia mwaka wa kwanza hadi sasa niko mwaka wa mwisho chuoni lakini sasa imefikia hatua simuoni kuwa wa kuvutia kwangu kwa sababu ananikera. Amekuwa akitishia kuachia picha na video zangu za utupu iwapo nitakataa kukubali ombi lake la kunioa, nifanyeje?” Mrembo huyo aliuliza ushauri wa watu kwenye ukurasa wa jamaa mmoja ambaye anaendesha kipindi cha kutafuta suluhisho kwa kutumiwa jumbe za faragha.

Watu kwenye ukurasa huo waligawanyika kwa maoni, baadhi wakionekana kumlimbikizia lawama mrembo huyo kwa kumuona mwanamume wake kama kinyaa baada ya kutumia gharama zake chuoni.

“Wanawake sio waaminifu na hata ukipata mwaminifu hisia zake zikibadilika atalalamika juu ya madhaifu aliyokuwa akikubali kisha kuachana. Maisha sio sawa kwa hivyo usiwe na usawa, uwe mtu wa kukasirisha,” Emanon alisema.

“Unasoma shule na mpenzi wako ndiye amekuwa akifadhili elimu yako. Sasa unasema unamwona hana mvuto na anakera, kuwa mkweli na wewe ehh una wazimu. Mwache akuachie uchi wako maana wewe si mtu mzuri. Haupaswi kuanza kile ambacho hautamaliza. Tafadhali kama mwanamke usiwahi kuanza usichomaliza,” IB Victan alimwambia.

“Kubali akuone ili asije akatoa uchi wako, Wakati wa ndoa, tafuta njia ya kumbukumbu yake na uifute. Kisha mtaliki baadae,” mwingine alimshauri.