Willy Paul ajibu uvumi kuhusu video yake na msichana Thika Road

Wakati mastaa wengi mara nyingi huchagua wanadada ambao ni maarufu na wanaopendeza, Willy Paul anajitokeza kuwa tofauti kwa tendo hilo kulingana na mashabiki wake.

Muhtasari

•Video iliyovuma  mtandaoni imezua hisia nyingi huku Wakenya wakifurahishwa na jinsi mwanamuziki huyo maarufu alivyomchukua mwanadada huyo.

Willy Paul alionekana akizungumza na msichana kando mwa barabara ya Thika na watumiaji wa mtandao hawakuchelewa kuanza udaku. 

Video iliyovuma  mtandaoni imezua hisia nyingi huku Wakenya wakifurahishwa na jinsi mwanamuziki huyo maarufu alivyomchukua mwanadada huyo.

Wakati mastaa wengi mara nyingi huchagua wanadada ambao ni maarufu na  wanaopendeza, Willy Paul anajitokeza kuwa tofauti  kulingana na mashabiki wake.

Wengine kwa haraka pia walimiminika kwenye sehemu ya maoni ili kutoa mawazo yao juu ya tukio hilo.

Haya ni baadhi ya maoni na hisia za watu kutokana na tukio hilo.

“Wakati nilipoona video hii kwenye TikTok nilikuwa kama, si hii gari ni ya pozze. 😂

“Mtandaoni mna sifu mali safi lakini kwa ground mna kula njahiii,” alisema mwingine.

“Afathali gloria muliro angeacha ajitie kitanzii 😂😂😂😂😂”

“Nivile tu huyu hakushuka nduthi . Willy Paul ni mkimbizi namba moja” yalisomeka maoni tofauti.

Willy Paul alionyesha kutopendezwa na hisia za baadhi ya mashabiki wake wa mtandaoni huku akisema kwa ucheshi  kwamba alikuwa akimjia mama wa mtu aliyechukua video hiyo. na kutangaza kuwa atatoa albamu nyingine.

"Lilikuwa tukio la kupendeza, ijayo ni mama ya mpiga picha nitabeba 😃 😊 😀 😄 albam kubwa inayopakia familia." Willy Paul aliandika.

 Willy Paul mapema mwaka huu aliwaonya wanaume wanaotoka kimapenzi na warembo wa Instagram ambao aliwataja kama kikombe chenye sumu na kwamba watafute wake vijijini.

“Jambo moja ambalo nimegundua ni kwamba hawa madem wa Instagram ni sumu. Wanaume wenzangu tutafute wife materials ushago, tuwasafishe wang'are vile tunataka. Hawa wa TikTok na IG ni mapepo. Dakika moja uko na yeye hapa Nairobi, dakika inayofuata ako na baba Kamau Mombasa na akabadilisha hadi jina,” aliandika.