Wewe ndio malkia wangu, roho yangu na kila kitu kwangu - Diamond kwa bintiye Tiffah

Ikumbukwe Oktoba mwaka jana, Tiffah alishurutishwa na wazazi wake kutia saini hati ya kukiri kutojihusisha kimapenzi hadi mwaka 2045.

Muhtasari

• Diamond alimsifia Tiffah kuwa ni malkia wa himaya yake ya Simba, akimwambia kwamba anampenda kuliko anavyompenda mtu yeyote.

Diamond na Tiffah
Image: INSTAGRAM// PRINCESS TIFFAH

Awali tuliripoti kwamba msanii Diamond Platnumz yuko nchini Afrika Kusini kwa ziara zake za kimuziki lakini pia alipata muda mzuri wa kuitembelea familia yake na kujumuika na wanawe na aliyekuwa mpenzi wake Zari, Nillan na Tiffah.

Katika haditih hiyo, Diamond aliweza kuwatembeza watoto wake kwenye makabrasha yake na kuwaonesha vito vya thamani anavyomiliki ikiwa ni pamoja na saa za dhahabu na mikufu ya dhahabu pia.

Sasa msanii huyo alikwenda kwenye jukwaa la Snapchat na kupakia video ya bintiye Tiffah na baba mtu alitokwa na maneno matamu ya kumsifia binti huyo aliyezaa na Zari.

Diamond alimsifia Tiffah kuwa ni malkia wa himaya yake ya Simba, akimwambia kwamba anampenda kuliko anavyompenda mtu yeyote.

“Huyu hapa, nampenda sana, huyu ni malkia wa roho yangu, nakupenda sana. Anajua kwamba nampenda Zaidi, huyu ni mtoto wangu, ndio binti mfalme, kila kitu kwangu, nampenda sana, jina lake ni Latiffah, lakini napenda kumuita Latty ama Tiffah Dangote,” Diamond alisema huku akimshika mkono binti yake.

Kwa upande wake, binti huyo mdogo alikuwa akijishaua na kujishebedua mbele ya babake kwa madaha na madoido.

Hii si mara ya kwanza Diamond anaonesha mapenzi yake kwa bintiye Tiffah.

Itakumbukwa mwezi Oktoba mwaka jana, binti huyo wa Zari na Diamond alishrutishwa na wazazi wake kutia mkataba wa kutojihusisha na mapenzi hadi mwaka 2045.

Tiffah alionekana kwenye video akiwa na kaka zake ambao walitoa ahadi yake ya kutokuwa na mpenzi hadi 2045.

Alitia saini hati hiyo kabla ya kwenda kusalimiana na kaka zake kwa mtindo sawa na mikataba ya biashara

"Siamini ni ndugu zangu wanaonifanya nitie sahihi mkataba huu," Tiffah aliandika kwenye ukurasa wake.