Silvanus Osoro ashangazwa nywele zake kumea na kuwa kubwa wiki tu baada ya kunyoa

“Hii nywele yangu huwa na mbolea walahi. Ndani tu ya wiki moja, imemea tena!!" Osoro alisema.

Muhtasari

• Osoro alihisi hivyo kwani alidai kwamba zinaota na kua kubwa kwa haraka ndani ya wiki moja tu baada ya kunyoa.

Silvanus Osoro, Mbunge wa South Mugirango na kiranja wa wengi kwenye bunge.
Silvanus Osoro, Mbunge wa South Mugirango na kiranja wa wengi kwenye bunge.
Image: Facebook

Mbunge wa Mugirango ya Kusini Silvanus Osoro ambaye pia ni kiranja wa wengi katika bunge la kitaifa ni mtu alyebarikiwa na nywele kweney kcihwa chake, kinyume na wengi wa rika lake ambao wanahaha kuficha vipara kwa kutumia kofia.

Mbunge huyo amezungumzia nywele zake kupitia chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii akisema kwamba anahisi nywele zake huwa na mbolea ya kiasili.

Osoro alihisi hivyo kwani alidai kwamba zinaota na kua kubwa kwa haraka ndani ya wiki moja tu baada ya kunyoa.

Mbunge huyo muongeaji na mtetezi mkali wa sera za uongozi wa rais Ruto alipakia picha hizo akiwa amevalia nadhifu na kuchukua nafasi hiyo kuwakaribisha Wakenya wote katika kaunti ya Kericho hapo Kesho ambapo sherehe za Mashujaa zitafanyika.

Hii nywele yangu huwa na mbolea walahi. Ndani tu ya wiki moja, imemea tena!! Lakini kwa wakati huo huo, fanya kile unachoweza kukifanya kidogo kidogo na kwa uzingatifu, utafika pale. Wewe ni shujaa. Tukutane Kericho tunywe chai,” Osoro alisema.

Osoro ni mbunge kwa mara ya pili katika eneo bunge lake na amekuwa akisemekana kwamba katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2027, huenda akajitosa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana wa kaunti ya Kisii kumenyana na gavana wa sasa Simba Arati.

 Osoro na Arati katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakitupiana cheche na lawama kuhudu uongozi wa kaunti hiyo yenye ukwasi wa ndizi, huku kwa wakati mmoja wakikabiliana vikali kwa kukunjana mashati wakati wa hafla ya mazishi ya babake aliyekuwa naibu gavana wa kaunti hiyo Joash Maangi.