Mulamwah asimulia kilichomfanya kujenga chumba cha kifahari kijijini

Millioni mbili ndio zimebaki kukamilisha nyumba yangu asema Mulamwah

Muhtasari

•Mimi ni kioo cha jamii ,familia mingi kwenye ukoo wetu zinanitegemea ndio maana nikafanya juhudi kujenga mjengo mkubwa kwa ajili yao

Mulamwah
Image: Facebook

Mchekeshaji mashuhuri wa Kenya David Oyando almaarufu Kendrick Mulamwah amefunguka na kusimulia kilichomfanya awe na maono ya kujenga Nyumba ya kifahari kijijini , ambayo amesema imegharimu mamilioni ya pesa.

"Maoni ya kujenga  kijijini nilitaka kufuata mfano wa babangu nikiwa mchanga  watoto wa wajomba wangu walifanikisha masomo yao kwa kuishi kwetu kwa maana babangu aliwapa makazi kwa kuwa na nyumba kubwa,"alisema.

Mulamwah alisimulia zaidi kuwa kujenga nyumba yake ni kwa ajili ya kusaidia wakiwemo ndugu,dada na amu zake wakati wanapohitaji huduma za makazi kwa maana anafahamu kule alikotoka na jamii inavyomtegemea.

Mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia ni muuguzi kwenye mahojiano alisimulia kukekwa na matusi ya wabea wakimtaja kuekeza kijijini kwa mjengo wa mamilioni ambayo angeekeza mjini kwa faida ya maisha yajayo.

"Nimepitia mengi kwenye mitandao ila kwangu nyumba yangu ndio faranja yangu wakati itakamilika najua itakuwa baraka kwa jamii yangu.

Mulamwah alisema kuwa nyumba hiyo imebakisha kiasi cha millioni  mbili ndiposa ikamilike huku akisema kuwa mipango ya kukamilisha inaendelea.