Bondia Anthony Joshua, 34, asema hajapata sababu ya kuondoka kwa mamake na kuoa

oshua alisema kwamba mrembo yeyote ambaye atapata bahati ya kuolewa naye basi anafaa kujiandaa kisaikolojia kwamba hakuji tu kuolewa na Joshua pekee bali ataolewa na familia yake yote.

Muhtasari

• 'Katika utamaduni wetu, tulikulia katika nyumba ya familia yetu wenyewe, tunawasaidia wazazi wetu.” - Joshua alisema.

Bondia Anthony Joshua na mamake
Bondia Anthony Joshua na mamake
Image: Instagram, BBC

Bondia wa Uingereza mwenye usuli wa Nigeria, Anthony Joshua amefichua ni kwanini bado anaishi na mama yake akiwa na umri wa miaka 34, akisisitiza kuwa mpenzi yeyote wa baadaye atapata shida kumshawishi kuhama.

Joshua, ambaye bado anaishi katika nyumba ya mamake yenye vyumba viwili vya kulala alisisitiza kwamba licha ya wengi kuona kwamba katika umri wake na kuzingatia mafanikio makubwa ambayo ameyapata hadi sasa katika mchezo wa ndondi, anafaa kuwa mwanamume wa kujitegemea na mwenye familia yake, kwake bado hajapata sababu au kishawishi cha kutosha kumchochea kuondoka kwa mamake na kuhamia kwa nyumba yake.

Bondia huyo wa Uingereza aliketi na mwanahabari wa BBC, Louis Theroux kujadili uhusiano wake wa karibu na familia yake na kuwaonya rafiki wa kike wa baadaye watahitaji kushindana na mama yake, Yeta Odusanya katika kupata umakini wake.

"Bado ninaishi na mama yangu," bingwa huyo wa dunia mara mbili aliambia BBC. 'Katika utamaduni wetu, tulikulia katika nyumba ya familia yetu wenyewe, tunawasaidia wazazi wetu.”

'Kwa nini nitahama na kumwacha mama yangu peke yake, kwa ajili ya msichana fulani? Familia ndio jambo muhimu zaidi.’

Kwa tahadhari, Joshua alisema kwamba mrembo yeyote ambaye atapata bahati ya kuolewa naye basi anafaa kujiandaa kisaikolojia kwamba hakuji tu kuolewa na Joshua pekee bali ataolewa na familia yake yote.

'Msichana atakapokuja kwangu kama mke wangu, yeye sio tu anaolewa na mimi, anaolewa  na familia yangu.'

Nyota huyo wa ngumi ambaye hayupo hadharani kwenye uhusiano, alikiri kuwa anapenda kuweka maisha yake binafsi kuwa ya faragha kwani hawezi kufikia matarajio ya watu kutoka kwake.