Tulimaliza ugomvi wetu na Harmonize kwa ajili ya vizazi vya kesho -Rayvanny

Rayvanny alimsifia Harmonize kwa tuzo za marekani huku akiwataja waliozikashifu kuwa watani tu

Muhtasari

•Msanii huyo alisimulia zaidi akisema kuwa kwa sasa yeye na Harmonize wekuwa marafiki wakubwa kila mara wanatembeleana ili kujuliana hali kwenye taaluma ya muziki

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE, RAYVANNY

Staa wa bongo Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny amefunguka kuhusiana  na ugomvi uliokuwepo kati yake na msanii Harmonize akisema kuwa walionelea ni vyema kuumaliza kwa manufaa ya vizazi vyao vya kesho.

"Harmonize tulikuwa naye pomoja kwa Lebo moja ila kuna tofauti zilitokea kati yangu naye kukawa na chuki kwa maana kila mmoja alijiona bora zaidi kuliko mwingine licha ya hayo yote kulifikia wakati tukaonelea ni vyema kumaliza ugomvi wetu, ndiposa tuwa mfano bora kwa wafuasi wetu na vizazi vyetu vya kesho,"alisema Rayvanny.

Msanii huyo alisimulia zaidi akisema kuwa kwa sasa yeye na Harmonize wekuwa marafiki wakubwa kila mara wanatembeleana ili kujuliana hali kwenye taaluma ya muziki.

"Mimi na Harmonize tumekuwa kama ndugu kwa maana kwa sasa tunaheshimiana,mara kwa mara tunakuta kujuliana hali na kuendelesha sanaa yetu mbele." Rayvanny aliongeza.

Rayvanny alimsifia Harmonize kwa tuzo tatu alizopewa Marekani huku akiwataja waliozikashifu kuwa watani tu.

Wengi kwenye mitandao walimchana Harmonize wakimtaja kuwa kanunua tuzo ila,hilo si kweli Harmonize alishinda tuzo hizo baada ya makabiliano makali aliibuka mshindi.

"Hakuna mtu anaweza kununua tuzo ili afurahishe wafuasi wake tuzo za Harmonize ni za kweli kwani kuna majimbo pia Marekani nilishinda tuzo licha ya kutokwenda huenda Harmonize akaniletea Tuzo yangu kwa kuwa tumekuwa marafiki,"alisema Rayvanny.