‘Respect the OGs’ Kalighraph amwambia Mudavadi hadharani

Kile kilichowachekesha mashabiki wake ni jinsi alivyomkaribisha Mudavadi na wanasiasa wenzake jukwaani.

Muhtasari

• Aliwapa nafasi ya kuzungumza ila wakasusa,huku wakisema kuwa wanataka kuburudishwa tu na muziki wa msanii huyo.

• “Respect the OG”

Kaligraph Jones
Kaligraph Jones
Image: Instagram

Msanii Khaligraph Jones alipata nafasi ya kujumuika pamoja na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi katika tamasha la kutumbuiza kwenye uzinduzi wa Cocacola Caravan kwa ajili ya sherehe za msimu wa Krisimasi.

Akiwa jukwaaani Kaligraph alimwalika waziri huyo wa mambo ya nje wakiwa na mwenzake waliyeandamana naye ili waburudike kwa muziki pamoja.

Aliwapa nafasi ya kuzungumza ila wakasusa,huku wakisema kuwa wanataka kuburudishwa tu na muziki wa msanii huyo.

“Respect the OG”, alisema Kaligraph baada ya wawili hao kukataa kuzungumza.

Kile kilichowachekesha mashabiki wake ni jinsi alivyomkaribisha Mudavadi na wanasiasa wenzake jukwaani.

Khaligraph alianza kwa kuvua kofia yake na kudai kwamba hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kupata nafasi ya kualika wanasiasa jukwaani lakini akasema atajaribu lakini kwa jinsi alivyojaribu ndio aliwaacha hoi wengi.

“Mpaka nimetoa kofia, samahani waheshimiwa, sijawahi fanya hili kabla, sijui jinsi ya kualika wanasiasa jukwaani. Lakini nitajaribu kufanya vizuri jinsi nijuavyo. Tafadhali, panda juu ya steji,” OG aliongea kwa sauti ya kutoa amri.

Musalia Mudavadi na mwenzake wakajongea jukwaani wakiwa wamevalia vilemba vya ‘father christmas’ kabla ya Khaligraph kuanza kuimba nao wimbo wa ‘Sifu Bwana’ – kolabo ya nguvu aliyomshirikisha Nyashinski mwaka mmoja uliopita na ikafanya vizuri ajabu.

Kwa wakati mmoja alimuuliza Mudavadi kama angetaka kuchukua kipaza sauti ili kuwaimbia mashabiki lakini waziri huyo kwa tabasamu na kucheka akasema hawezi.