Harmonize adokeza mpango wa kumtambulisha msanii mpya Konde Gang hivi karibuni

“Kwa hiyo ukifika muda rasmi wa kutangazwa msanii wa Konde Music, atatangazwa na naamini atafanya vizuri kwa sababu siku hadi siku unajua tunajifunza vitu," alisema.

Muhtasari

• Wengi walitafsiri kwamba Dvoice ni mrithi wa viatu vya Rayvanny aliyeondoka kwenye lebo pia mwaka jana.

• Itakumbukwa Novemba 16 Diamond alimtambulisha msanii Dvoice kwenye lebo kama msanii was aba tangu lebo ya WCB Wasafi izinduliwe mwaka 2016 mwezi Februari.

Harmonize
Harmonize
Image: Screengrab

Msanii Harmonize amedokeza kwamba lebo yake ya Konde Music Worldwide ina mpango wa kusaini msanii mpya lakini hawataweza kufanya hivyo kwa sasa kwa sababu wanajaribu kuepuka dhana kwamba wanataka kuleta ushindani na lebo ya Diamond ambao wiki mbili zilizopita walitambulisha msanii wao – Dvoice.

Akizungumza na blogu moja nchini Tanzania, Harmonize alifichua kuwa kuna msanii mpya na ambacho kimesalia ni kumtambulisha tu na kuanza kuachia miziki yake.

Alisema kwamba amejifunza mengi kutokana na sajili za awali zilizobuma kutoka kwa wasanii Killy, Cheed na Anjella lakini akasema kwamba bado hilo halitamzuia kuendelea kuwashika mkono vijana wengine.

“Siku hadi siku ninakua na najifunza vitu, naamini kabisa hata msanii mpya akitambulishwa hakutakuwa kama mwanzo, kutakuwa vitu vimebadilika, kwa hiyo kutakuwa na wasanii ila kwa sasa sitaki ionekane kama inatumika kisiasa au kimashindano.”

“Kwa hiyo ukifika muda rasmi wa kutangazwa msanii wa Konde Music, atatangazwa na naamini atafanya vizuri kwa sababu siku hadi siku unajua tunajifunza vitu kwa sababu haikuwa rahisi hata kufika hapa,” alimaliza.

Itakumbukwa Novemba 16 Diamond alimtambulisha msanii Dvoice kwenye lebo kama msanii was aba tangu lebo ya WCB Wasafi izinduliwe mwaka 2016 mwezi Februari.

Wengi walitafsiri kwamba Dvoice ni mrithi wa viatu vya Rayvanny aliyeondoka kwenye lebo pia mwaka jana.