Fahamu mastaa ambao wanatarajiwa kufunga pingu za ndoa ya maisha mwezi Desemba

Wanandoa hawa wako tayari kula viapo mbele ya mashabiki wao kuahidi kuwa na upendo usioyumba.

Muhtasari

• Wengine huratibisha mwezi huu kuwa spesheli  ambapo wanafanya hatua muhimi za maisha.

• wanandoa hawa wako tayari kula viapo mbele ya mashabiki wao  kuahidi kuwa na upendo usioyumba.

Mastaa ambao wanatarajia kufunga ndoa mwezi Desemba 2023
Mastaa ambao wanatarajia kufunga ndoa mwezi Desemba 2023
Image: INSTAGRAM

Mwezi wa Disemba,umejaa umuishwa na sherehe za misimu mbalimbali hasa za kufunga mwaka , familia na marafiki hukutana katika maeneo tofauti ili kuidhinisha sherehe hizo.

Wengine huratibu mwezi huu kuwa spesheli  ambapo wanafanya hatua muhimi za maisha.

Wanandoa watatu maarufu nchini Kenya  wamechagua mwezi huo wa Desemba kuwa mwanzo wa  kuanza safari ya upendo wa milele.

Katika onyesho la kupendeza na lenye mahaba, wanandoa hawa wako tayari kula viapo mbele ya mashabiki wao  kuahidi kuwa na upendo usioyumba.

Wafuatao ni wapenzi ambao watafunga ndoa mwezi Desemba, 2023.

  1. Kevin Kioko (Bahati) na mkewe Diana Marua.

Msanii  Kevin Kioko, maarufu kama Bahati, awali alitangaza kwamba tarehe 12 Desemba 2023 itakuwa siku ambayo yeye na Diana Marua wangebadilishana viapo vyao rasmi.

Mnamo Juni, Bahati  alishiriki habari hizo kwa furaha akisema, "Alisema ndio, na ninatangaza rasmi kwamba tarehe 12 Desemba 2023 ni siku ya harusi yetu."

Wapenzi hawa awali walifanya  sherehe za kitamaduni  (uracio) kuidhinisha kumbukumbu ya mika saba wakiwa kwenye mahusiano.

  1. Nicholas Kioko na Ashley

Baada ya kuwakaribisha mapacha wao kwa furaha mwezi wa Februari, mwanablogu maarufu Nicholas Kioko na mpenzi wake mpendwa, Ashley, waliongeza sura nyingine ya msisimko katika safari yao pamoja. Walitangaza kwa furaha kwamba watakuwa wakibadilishana viapo mwezi  wa Desemba.

Katika cahpisho lao la mwaliko wapenzi hawa walifichua kuwa harusi yao imepangwa kufanywa Desemba 29,2023.

Mwaliko huo ulisomeka kwa uzuri, “N. Kioko na Ashley wanakualika kwa moyo mkunjufu ujiunge nao kwa sherehe ya arusi yao siku ya Jumamosi, tarehe 29 Desemba 2023, saa 10:00 asubuhi.”

  1. Mummie Francie na Godfrey Andy

TikToka Mummie Francie alishiriki habari za kusisimua anapojiandaa kwa ajili ya harusi yake ya pili ya kitamaduni, inayotarajiwa kufanywa Desemba 24, 2023,sawia naya mwaka jana.

Francisca Mbaye,( Mummie Francie) aliadhimisha safari yake ya ndoa mwaka jana kwa harusi ya kitamaduni katika Kijiji cha Namutsula katika mji wa Matayos, Kaunti ya Busia.

Vile vile, mwaka huu, Mummie alitumia akaunti yake ya TikTok kutangaza, "Siamini kwamba historia itajirudia mwaka huu, tarehe sawa lakini eneo tofauti-Tanzania, ardhi ya mama yangu," alisema.