Kuwekwa si dhambi, 50 ya kupewa ni tamu kuliko 50 ya kujitafutia - Manzi wa Kibera

"Hakuna pesa tamu kama ya mwanamume, ile ya kupewa hivi hata kama ni 50 bob huwa tamu sana. Shilingi 50 ya kupatiwa bure ni tamu kuliko ile 50 ambayo umefanyia kazi,”

Muhtasari

• Aliwashauri wanadada kwamba wasijaribu karata ya kuwaweka wanaume kwani wanaume ndio wanafaa kuweka warembo.

Manzi wa Kibera
Manzi wa Kibera
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera amefunguka kuhusu ‘kuwekwa’ na mzee wa miaka 67 bila kugharamika chochote.

Mrembo huyo katika mahojiano na SPM Buzz, aliweka wazi kwamba mzee wake wa miaka 67 ndiye alimhamisha kutoka Kibera na kumbadilishia maisha katika mazingira mazuri.

Alisema kwamba licha ya uvumi wa kuachana, bado mzee huyo ndiye anamlipia kodi ya kila mwezi licha ya kwamba hawajawahi ishi pamoja, huku pia akifichua kuwa kuna wakati mmoja mzee huyo alijaribu kukataa kulipa kodi nusra amchukulie hatua za kisheria.

“Bado ni yeye analipa kodi, kwani nani anafaa kulipa, na si tafadhali, buda ni mwisho wa mwezi changamka. Nampigia namwambia niaje landlord ananisumbua, simu yangu inalipuka kupigiwa simu, changamka. Mwezi wa kwanza hadi 3 alikuwa sawa lakini hapo akajaribu kuleta kichwa ikabidi kidogo nimpeleke mbele ya sheria. Hatujawahi ishi na yeye hapa, yeye hukuja tu vile mimi naenda kwake pia,” Manzi wa Kibera alisema.

Manzi wa Kibera pia alikiri kwamba mzee huyo ndiye anayemfanyia kila kitu, akisema kwamba kuwekwa ni tamu kuliko kujisimamia katika kila kitu.

“Kuwekwa sio dhambi, ukipata vitu vya bure teremka navyo, Nairobi ni kubaya, rais ametukalia kwa hiyo hata sisi ni lazima tukaliane hapa nje. Mwanamke hula katika pande mbili; kwa mwanamume na kwa biashara yake. Hakuna pesa tamu kama ya mwanamume, ile ya kupewa hivi hata kama ni 50 bob huwa tamu sana. Shilingi 50 ya kupatiwa bure ni tamu kuliko ile 50 ambayo umefanyia kazi,” Manzi wa Kibera alibainisha.

Aliwashauri wanadada kwamba wasijaribu karata ya kuwaweka wanaume kwani wanaume ndio wanafaa kuweka warembo.