Akothee ampa mwanafunzi wa chuo kikuu hundi ya shilingi elfu 50 za matumizi binafsi

Akothee akizungumzia safari yake ya masomo, alisema kwamba hatimaye atakamilisha safari yake ya kuifukuzia digrii ya kwanza baada ya miaka 14 ya kufanya hivyo.

Muhtasari

• Itakumbukwa kuwa Akothee ni mmoja wa wanafunzi ambao wanatarajiwa kufuzu kutoka chuo hicho mapema mwezi ujao wa Desemba.

Akothee
Akothee
Image: Facebook

Siku chache tu baada ya kutangaza kwamba atakuwa anawapa mashabiki wake shakiki zawadi za hadi shilingi milioni moja kwa kumuunga mkono kwa muda wote kuanzia Desemba mosi, Akothee ameanza kwa kumpa mwanafunzi mmoja shilingi elfu 50 kwa ajili ya matumizi ya binafsi.

Taarifa hizi hazikufichuliwa na Akothee bali zilifichuliwa na chuo cha Mount Kenya na kusema kwamba Akothee alimpa hundi mwanafunzi wa kike wa chuo hicho ambaye amekuwa akipitia maisha magumu kwa kukosa hela za matumizi ya vitu vidogo vidogo.

“Mtu mashuhuri Akothee amempa mwanafunzi wa Mafunzo ya matibabu wa MKU, Milly Nafula KSh50,000 za kumtunza. Akothee alikabidhi hundi hiyo kando ya kongamano la kiamsha kinywa kuhusu ufadhili wa masomo na ufadhili wa elimu, ambalo liliandaliwa na MKU Foundation katika hoteli moja Nairobi mnamo Jumatano, Novemba 29, 2023. Milly kwa sasa anasomea bachelor of medicine na bachelor of surgery chini ya udhamini kamili wa MKU Foundation,” taarifa hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wa MKU Facebook.

Itakumbukwa kuwa Akothee ni mmoja wa wanafunzi ambao wanatarajiwa kufuzu kutoka chuo hicho mapema mwezi ujao wa Desemba.

Akothee akizungumzia safari yake ya masomo, alisema kwamba hatimaye atakamilisha safari yake ya kuifukuzia digrii ya kwanza baada ya miaka 14 ya kufanya hivyo.

Alisema kwamba alilazimika mara si moja kuweka azma yake ya kutafuta Digrii pembeni ili kutoa fursa katika kuwasaidia wengine kutoka kwa jamii na familia zisizo na uwezo wa kukimu mahitaji ya karo.

Pia Akothee amezindua shule yake ya msingi ambayo mwaka jana akitangaza ndoto hiyo, alisema itampa nafasi murwa ya kunyoosha mkono wake kwa kutoka elimu kwa watoto kutoka familia maskini kwa kuwapa elimu ya msingi yenye kuwawezesha angalau kujua kusoma na kuandika.