Msanii Dvoice amsifu Diamond kwa ya kumzawadi mikufu na pete vya dhahabu

Diamond anapenda kuzingatia wafanyikazi wake wawe na maisha bora Dvoice asema.

Muhtasari

•Msanii Dvoice alitabulishwa kwenye Lebo la Wasafi mwezi Novemba chini ya usimamizi wa mkurugenzi mkuu Diamond Platnumzs

Dvoice na Diamond
Dvoice na Diamond
Image: Screengrab, Instagram

Nyota mpya kwenye Lebo la Wasafi msanii Dvoice siku chache baada ya kutambulishwa rasmi amemsifia bosi wake Diamond Platnumz kwa zawadi nyingi zikiwemo pete za dhahabu mikufu na hata mavazi.

Msanii Dvoice aliyasema hayo kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanahabari wa kituo cha Wasafi FM alipokuwa akielezea jinsi maisha yake na muonekano umebandilika chini ya uongozi wa mkurugenzi mkuu wa Wasafi Diamond Platnumz.

"Kwa kweli Diamond ni msanii ambaye anapenda kushirikiana na wafanyikazi wake vyema kuhakikisha kuwa wakati wanapofanya shoo au mahojiano mavazi na muonekano wao uwe bora na wa mvuto, mimi ni mmoja woa nilishangaa kuona jinsi alivyo mkarimu baada ya kunikabidhi pete mbili za dhahabu zenye thamani ya Tsh 42,000,000 (Ksh 2,573,950),"alisema Dvoice.

Kulingana na Dvoice siku chache ambazo amekuwa kwenye Lebo la Wasafi msanii Diamond amekuwa na upendeleo kwake kwa kuwa amempa   viatu  vya thamani  ya juu, mikufu asili ambayo wasanii wengi hawawezi kumiliki.

Dvoice alielezea zaidi kuwa kutambulishwa kwake kwenye Lebo ya Wasafi kumekuwa kwa manufaa zaidi kwa taaluma yake kwenye muziki wa Bongo kwa jinsi ambavyo amepokelewa kwa upendo na heshima.