Diamond ahuzunika baada ya shabiki akiiba kofia yake ya kijani

Aliendelea kuelekeza sehemu ya ulinzi wake kubaki nyuma na kutafuta kofia.

Muhtasari
  • Diamond alisimama kwa muda baada ya kofia yake kuchukuliwa lakini timu yake ya ulinzi ilimuongoza hadi kwenye gari huku wengine wakiendelea kumtafuta mwizi huyo ‘mdogo’.

Mwimbaji wa Bongo Diamond Platinumz aliachwa na huzuni baada ya shabiki kuiba kofia yake ya kijani.

Tukio hilo lilitokea mjini Dodoma, wakati wa kikao na mashabiki wake.

Kulingana na video ambayo imekuwa ikisambazwa sana mtandaoni, Diamond na timu yake walikuwa wakipita katikati ya umati mkubwa wakati mmoja wa shabiki wake mtukutu alipomfikia kichwani, akivua kofia yake. Shabiki huyo alitoweka mara moja kwenye umati.

Diamond alisimama kwa muda baada ya kofia yake kuchukuliwa lakini timu yake ya ulinzi ilimuongoza hadi kwenye gari huku wengine wakiendelea kumtafuta mwizi huyo ‘mdogo’.

"Kofia lazima ipatikane kwa nguo nyingi," Diamond aliambia usalama wake. Yaani nguo zote zinzokuja navalia kofia hilo, sa mimi nitaavaje leo,”

Aliendelea kuelekeza sehemu ya ulinzi wake kubaki nyuma na kutafuta kofia.

Kofia hiyo hatimaye ilipatikana na kurudishwa kwa mmiliki wake halali kupitia usaidizi wa mmoja wa wenyeji. Kofia hiyo ilikutwa mikononi mwa boda ambao kila mmoja alikuwa akiijaribu.

Diamond aliyefarijika alisema kuwa kofia hiyo ilikuwa ya kawaida tu na hata haikuwa ghali.

Ni tukio ambalo liliwaacha wengi wa mashabiki wake wakimkejeli.