Lilian Nganga afichua alipogundua kuwa ana ujauzito wa Juliani

Mwimbaji Juliani na Lilian Nganga wana mtoto wa kiume wa kupendeza anayeitwa Utheri.

Muhtasari
  • " Niligundua nilikuwa mjamzito tarehe 2 Desemba 2021. Miaka 2 imepita na ni ukamilifu! Furaha mama!" Aliandika.
Lilian Ng'ang'a

Kupitia kwenye ukueasa wake wa instagram mpenziwe Juliani Lilian Nganga amefichua alipopata kuwa ana ujauzito wa mwanawe wa kwanza.

Lilian ameweka wazi kwamba ana furaha kuwa mama, kwani imekuwa safari ya ajabu.

" Niligundua nilikuwa mjamzito tarehe 2 Desemba 2021. Miaka 2 imepita na ni ukamilifu! Furaha mama!" Aliandika.

Mwimbaji Juliani na Lilian Nganga wana mtoto wa kiume wa kupendeza anayeitwa Utheri.

Lilian Nganga aliolewa na Waziri wa Mawaziri Alfred Mutua kwa miaka kumi kabla ya kutengana.

Wanandoa hao walitangaza kutengana mnamo Agosti 2021 na muda mfupi baadaye alitangaza uhusiano wake na Julius Owino ambaye anajulikana kama Juliani.

Wapenzi hao wawili walikabiliwa na shutuma nyingi na vitisho vya hadharani walipoanza kuchumbiana na Lilian alidhihakiwa kwa kumuacha mwanasiasa tajiri kwenda kuwa na rapa wa Kenya.

Wapenzi hao wawili walifunga ndoa ya kibinafsi mnamo Februari 2022. Lilian Nganga na Juliani hata walihudhuria sherehe ya miaka 51 ya kuzaliwa kwa Alfred Mutua pamoja.