Michael Olunga amwandikia mpenziwe ujumbe mtamu anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Hivi majuzi wanandoa hao waliishtaki kampuni moja ya majengo ya jiji kuhusu mzozo wa shamba la Ksh67 milioni.

Muhtasari
  • Mwanasoka huyo hapo awali alimtambulisha Grace kwa mashabiki wake mwaka wa 2019 kupitia Instagram yake.

Mwanasoka wa Kenya Michael Olunga ameandika ujumbe mzito  na wenye mahaba tele kumtakia mpenzi wake Grace Edith Akinyi siku njema ya kuzaliwa.

Mshambulizi huyo nyota ambaye kwa sasa anachezea Klabu ya Al-Duhail ya nchini Qatar, alieleza mapenzi yake kwa mpenzi wake huyo.

"Leo, malkia alizaliwa. Happy birthday love. Alikuwa akikutakia ushindi zaidi, afya, ustawi na furaha. Huu ni mwaka mwingine wa matukio, vicheko, na upendo usio na mwisho," Olunga aliandika.

Mwanasoka huyo hapo awali alimtambulisha Grace kwa mashabiki wake mwaka wa 2019 kupitia Instagram yake.

Hivi majuzi wanandoa hao waliishtaki kampuni moja ya majengo ya jiji kuhusu mzozo wa shamba la Ksh67 milioni.

Mwanasoka huyo alidai kuwa baada ya kufanya malipo hayo, kampuni hiyo ilikataa kuhamisha shamba hilo, hali iliyopelekea Olunga kushuku mpango wa ulaghai.