Muziki wake uliniponya kwa njia nyingi-Kambua asema huku akimuomboleza msanii Zahara

Mwimbaji huyo alifariki katika hospitali ya kibinafsi ya Johannesburg Jumatatu usiku akiwa na umri wa miaka 36 tu.

Muhtasari
  • Miongoni mwa hao ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Kambua.
Zahara
Zahara
Image: Instagram//ZaharaSA

Jumbe za rambirambi zimezidi kumiminika kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya msanii kutoa Afrika Kusini Zahara.

Miongoni mwa hao ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Kambua.

Kambua alienda kwenye mitandao yake ya kijamii kuomboleza mwimbaji huyo akisema

"Siku nyingine ya kuomboleza kuondokewa na mwanamke niliyempenda lakini sikuwahi kukutana naye @zaharasa. Nimesikitishwa sana na taarifa za kifo chake. Sijawahi kusikia sauti kama yake. Muziki wake umeniponya kwa njia nyingi. Treni uliyoimba kuhusu (Loliwe) hatimaye ilifika… pumzika vizuri Zahara. Asante kwa kushiriki zawadi yako nasi. Ulipendwa, na hazina kama hii kwa Afrika 🤍🕊️"

Mwimbaji huyo alifariki katika hospitali ya kibinafsi ya Johannesburg Jumatatu usiku akiwa na umri wa miaka 36 tu.

Mchumba Mpho Xaba alikuwa kando ya kitanda chake, jarida la Sunday World kutoka nchini humo limeripoti.

Hitmaker huyo wa kibao cha Loliwe alilazwa hospitalini akiwa na matatizo ya ini wiki mbili zilizopita. Chanzo kilicho karibu kiliiambia Sunday World kuwa mwimbaji huyo alifariki dunia kabla ya saa tisa alasiri.

“Familia itatoa taarifa hivi karibuni. Alikuwa na Mpho alipoaga dunia,” kiliongeza chanzo hicho.

Msemaji wa familia ya Mkutukana na binamu yake Zahara Oyama Dyosiba walisema alikuwa anatatizika kumpata Xaba Jumatatu usiku.

"Ninapokea simu kutoka kila mahali. Niko Cape Town na ninajitahidi niwezavyo kumpata Mpho. Siwezi kumfikia,” aliongeza.

Zizi Kodwa, waziri wa michezo, sanaa na utamaduni nchini humo, alichapisha kwenye X: “Nimehuzunishwa sana na kifo cha @ZaharaSA. Pole zangu za dhati kwa familia ya Mkutukana na tasnia ya muziki ya Afrika Kusini.

“Serikali imekuwa na familia kwa muda sasa. Zahara na gitaa lake walifanya mambo ya ajabu na ya kudumu katika muziki wa Afrika Kusini,” alisema Kodwa.

Wiki moja iliyopita, familia ilithibitisha kuwa Zahara alilazwa hospitalini kwa wiki moja.