"Nashangaa ninapokutazama" Esther Musila amsifia mumewe

Mama huyo wa watoto watatu alisifu sauti ya mume wake pamoja na tabasamu lake.

Muhtasari
  • Uhusiano wa wanandoa umekuwa ukichunguzwa vikali, lakini wamekiuka vikwazo vyovyote ili kuimarisha uhusiano wao.
mnamo siku ya harusi yao Januari 2022.
Esther Musila na mumewe Guardian Angel mnamo siku ya harusi yao Januari 2022.
Image: INSTAGRAM

Esther Musila amemlimbikizia sifa  mumewe mwanamuziki wa nyimbo za Injili Guardian Angel.

Mama huyo wa watoto watatu alisifu sauti ya mume wake pamoja na tabasamu lake.

Aliongeza Guardian ndio kila kitu alichotaka, akihitimisha ujumbe wake kwa kukiri kumpenda.

"Sauti yako ni muziki masikioni mwangu, tabasamu lako ni uzuri kwa macho yangu, ninashangaa ninapokutazama. Sio tu kwa sababu ya sura yako lakini kwa sababu ya kila kitu ambacho nimewahi kutaka kiko mbele yangu, nakupenda G,” alisema.

Guardian Angel alijibu chapisho lake kwa kutoa maoni na hisia kadhaa za mapenzi.

Uhusiano wa wanandoa umekuwa ukichunguzwa vikali, lakini wamekiuka vikwazo vyovyote ili kuimarisha uhusiano wao.

Musila pia amekuwa akiwapigia makofi wanamtandao ambao wamekuwa wakimnyatia kwa sababu ya kuolewa na mwanamume ambaye ni mdogo sana kwake.

Wanandoa hao mara nyingi hupostiana kwenye mitandao yao ya kijamii na kuandikiana jumbe tamu, ishara tosha kuwa wamefurahishwa sana na ndoa yao. Licha ya wengi kuwafurahia na kuwasherehekea, hawajakosa wenye chuki na wakosoaji ambao hutoa maoni hasi kwenye machapisho yao ya mitandao ya kijamii.