'Juzi tu nilikuwa polygamous sasa niko single' - Samidoh athibitisha kuachwa na Nyamu, Edday

Samidoh ni baba wa watoto 5, watatu na mke wa kwanza Edday Nderitu ambaye alihamia Marekani miezi kadhaa iliyopita, na 2 na seneta Nyamu ambaye hivi majuzi wameacha kufuatana Instagram,

Muhtasari

• “Juzi tu nilikua a polygamous man sasa niko single,” baba wa watoto watano alisema huku kukiwa na vicheko kutoka kwa marafiki zake.

Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Image: Instagram

Huenda msanii Samuel Muchoki, maarufu kama Samidoh ambaye pia anajiongeza kama afisa wa polisi, amethibitisha kuachwa na babymama wake wote wawili.

Samidoh juzi katika kipindi cha moja kwa moja na mashabiki wake kwenye Instagram alitoa tamko la kudokeza kuwa sasa amebaki bila mpenzi baada ya kutamba mitaani kwa kuwa mwanamume mwenye wake wawili kwa wakati mmoja miezi michache iliyopita.

Kwa mzaha alisema kwamba alikuwa ameondoka ghafla kutoka kuwa mtu wa wanawake wawili hadi kuwa mseja.

“Juzi tu nilikua a polygamous man sasa niko single,” baba wa watoto watano alisema huku kukiwa na vicheko kutoka kwa marafiki zake.

Wanamtandao walichukua maoni ya msanii huyo kama ujumbe wa uthibitisho kwamba hakuwa tena na uhusiano wa kimapenzi na seneta Karen Nyamu.

Samidoh amekuwa akituma ishara kuashiria kuwa uhusiano huo uliharibika haswa kupitia kujibu maoni chini ya chapisho lake na wanamtandao.

Hivi majuzi aligonga vichwa vya habari mitandaoni baada ya kumkashifu shabiki mmoja aliyedai kuwa mwanamuziki huyo ni mtu “mchungwa” anayemtegemea Nyamu kwa msaada wa kifedha.

Nyota huyo alijibu na kutangaza kwamba tayari alikuwa ameondoka nyumbani kwake na kuwashauri wanaume wengine kujaribu bahati yao.

Hapo jana Jioni, msanii huyo alitoa maoni ambayo wengi waliyatafsiri kuwa ya kumtusi seneta huyo.

Shabiki mmoja aliuliza kwa nini mwanamuziki huyo hakujibu mapenzi aliyopewa na Nyamu akimshutumu Samidoh kwa kutumia ushawishi wa kisiasa wa Nyamu kama hatua ya kumfikia.

Nyota huyo wa Mugithi alijibu madai kuwa Nyamu atalazimika kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa kwanza kwani bado hakuwa nao.

Haikushangaza basi kwamba mwanamtandao huyo alichukua matamshi yake kama msumari wa mwisho kwenye jeneza kama dhibitisho kwamba kwa hakika kulikuwa na shida peponi.

Nyamu amekuwa kimya zaidi kuhusu suala hilo kwani hajalishughulikia wala hajazungumza kuhusu maoni ya Samidoh ambayo sasa yanavuma mtandaoni.