Wafahamu maceleb wako waliobarikiwa na watoto 2023

Mjasiriamali huyo alishindwa kuzuia furaha yake alipokuwa akitangaza habari njema mtandaoni.

Muhtasari
  • Ni furaha ya kila mama kuona mwanawe baada ya kumbeba kwa miezi tisa, na kutoka kwenye chumba cha kuzalia akiwa hai na mwenye afya.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Image: Instagram

Mwaka huu watru mashuhuri,waigizaji,wasanii,wachekeshaji, miongoni mwa wengine waligonga vichwa vya habari kwa mambo tofauti.

Baadhi yao waliweza kubarikiwa na watoto huku wengine ikiwa ni mara yao ya kwanza kabisa kuwa wazazi na wengine wakiongeza na kupanua familia.

Ni furaha ya kila mama kuona mwanawe baada ya kumbeba kwa miezi tisa, na kutoka kwenye chumba cha kuzalia akiwa hai na mwenye afya.

Katika makala haya tutaangazia na kuorodhesha watu mashuhuri ambao walibarikiwa na watoto mwaka wa 2023.

1.Eric Omondi na Lynn Njihia

Mchekeshaji maarufu na mpenziwe Lynn walimkaribisha mwana wao wa pili mwaka huu, hii ni baada ya Lynn kuharibikiwa na ujauzito wa kwanza.

Eric Omondi kutambulisha sura ya mwanawe.
Eric Omondi kutambulisha sura ya mwanawe.
Image: Instagram

Wawili hao walibarikiwa na mtoto mrembo wa kike.

2. Nyce Wanjeri na Letting

Mwigizaji Nyce na mumewe walibarikiwa na mtoto ambaye anaitwa pendo Julai 12 mwaka huu,lakini walitangaza habari hizo njema kwa mashabiki kupitia mitandao yao ya kijamii Julai 14.

NYCE WANJERI NA MPENZIWE LETING KIPKEMBOI
Image: NYCE WANJERI/INSTAGRAM

3.Amber Ray na Kennedy Rapudo

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray alishiriki habari za mtoto wake kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Mei 15,2023.

Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Image: Instagram

4.Vera Sidika na Brown Mauzo

Mjasirimali Vera na aliyekuwa mpenzi wake Mauzo walimkaribisha mtoto wao wa pili Machi anayefahamika kama Ice Brown.

5. Wangari Thiongo  na Jimal Roho Safi

Wakisherehekea ujio wa mtoto wao mnamo Machi, Wangari Thiongo na Jimal Roho Safi walimtaja binti yao Amal J. Ibrahim.

 Wenzi hao walikuwa wameshiriki tangazo la ujauzito wiki mbili zilizopita, na Siku ya Wapendanao, 2023, walifichua uhusiano wao hadharani.

Huyu ni mtoto wa pili wa Wangari na mtoto wa tatu wa Jimal.

6.Carey Priscillah & Benito Muriu

Msanii wa vipodozi Carey Priscilla alishiriki furaha yake baada ya kumkaribisha mtoto wake mchanga mnamo Januari 2023, akimaliza safari yake ya ujauzito akiwa imara na mwenye afya njema.

Mjasiriamali huyo alishindwa kuzuia furaha yake alipokuwa akitangaza habari njema mtandaoni.