'Nimekuja kufanya amani,'Jalang'o asema baada ya kutembelea kaburi la baba yake

Katika video kadhaa zilizoshirikiwa kwenye Instastories zake, Jalang'o alionyesha ardhi yenye miti mingi ambapo baba yake na nyanyake wamezikwa.

Muhtasari
  • Hata hivyo, baada ya muda, alisema kwamba kila mtu katika nyumba hiyo aliondoka na kujenga nyumba zao mahali pengine, na kuacha ardhi bila kutunzwa na ukiwa.
Mbunfe Jalang'o asema hajutii kuutana na rais
Mbunfe Jalang'o asema hajutii kuutana na rais
Image: Instagram

Mbunge wa Lang'ata Felix Odiwuor, almaarufu Jalang'o, alitembelea kaburi la babake siku ya Krismasi na ahidi kulitengeneza.

Katika video kadhaa zilizoshirikiwa kwenye Instastories zake, Jalang'o alionyesha ardhi yenye miti mingi ambapo baba yake na nyanyake wamezikwa.

Alifichua kuwa shamba hilo lilikuwa la babu yake, na kuongeza kuwa aliishi hapo na familia yake alipokuwa mdogo.

"Hapa palikuwa nyumbani kwa babu yangu... ameaga... na nyumba yetu ilikuwa mahali fulani ... na wajomba zangu na kaka za baba yangu, hii ilikuwa nyumbani kwetu," alisema mbunge huyo kwenye video aliyoshiriki kwenye ukurasa wa Instagram.

Hata hivyo, baada ya muda, alisema kwamba kila mtu katika nyumba hiyo aliondoka na kujenga nyumba zao mahali pengine, na kuacha ardhi bila kutunzwa na ukiwa.

"Kila mtu amehama na kujenga nyumba yao katika eneo tofauti lakini eneo hili limesalia kuwa mahali maalum sana kwangu. Nimekuja kuleta amani na mzee wangu," Jalang'o aliongeza.